HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 4 December 2013

BARCLAYS PREMIER LEAGUE “Chamack wa Arsenal Aibeba Palace”



Chamack akifunga jana

MENEJA mpya wa Crystal Palace Tony Pulis amepata ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu England walipoifunga West Ham Bao 1-0 Jana Usiku.
Bao hilo la ushindi lilifungwa na Marouane Chamakh kwa kichwa katika Dakika ya 42 baada ya kuunganisha krosi ya Barry Bannan.
Palace wangeweza kufunga Bao nyingi kama si uhodari wa Kipa Jussi Jaaskelainen kuokoa Mipira miwili ya Jason Puncheon na Cameron Jerome.
Ushindi huu umewatoa Crystal Palace mkiani na kupanda juu ya Sunderland iliyobaki mwisho kabisa.
Mechi hii ilikwisha kwa rabsha pale Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Ravel Morrison, anaesifika kwa utukutu, kumsukuma Beki wa Palace Joel Ward kwa mkono usoni wakati Mpira umekwisha na Refa kumpa Kadi ya Njano ambayo itamfanya aikose Mechi ijayo ya West Ham dhidi ya Liverpool kwa vile amekusanya jumla ya Kadi za Njano 5 na hivyo kufungiwa Mechi moja.
Leo Usiku zipo Mechi 9 za Ligi Kuu England.
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Ward, Gabbidon, Delaney, Moxey, Jedinak, Dikgacoi, Bannan, Puncheon, Chamakh, Jerome
West Ham: Jaaskelainen, O'Brien, Collins, Tomkins, Rat, Noble, Nolan, Morrison, Downing, Diame, C.Cole
++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatano Desemba 4
22:45 Arsenal v Hull City
22:45 Liverpool v Norwich
22:45 Man United v Everton
22:45 Southampton v Aston Villa
22:45 Stoke v Cardiff
22:45 Sunderland v Chelsea
22:45 Swansea v Newcastle
23:00 Fulham v Tottenham
23:00 West Brom v Man City
++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
13
17
31
2
Chelsea
13
13
27
3
Man City
13
25
25
4
Liverpool
13
9
24
5
Everton
13
8
24
6
Newcastle
13
1
23
7
Southampton
13
6
22
8
Man United
13
5
22
9
Tottenham
13
-3
21
10
Hull
13
-4
17
11
Aston Villa
13
-1
16
12
West Brom
13
-1
15
13
Swansea
13
-2
15
14
Norwich
13
-12
14
15
West Ham
14
-3
13
16
Stoke
13
-6
13
17
Cardiff
13
-9
13
18
Fulham
13
-13
10
20
Crystal Palace
14
-14
10
19
Sunderland
13
-16
8

No comments:

Post a Comment