HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 22 November 2013

ZITTO KABWE AZUA ZOGO CHADEMA”UTATA SHUTUMA VYAMKABILI”




Dar es Salaam.
Suala la hatma ya Naibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe ndilo lililotawala katika siku ya pili ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na kusababisha mvutano mkali miongoni mwa wajumbe.
Pamoja na ukweli kuwa kulikuwa na ajenda kadhaa zilizokuwa zimepangwa kujadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika Dar es Salaam, suala la Zitto ndilo lililochukua muda mrefu zaidi kujadiliwa.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa wajumbe waligawanyika makundi mawili, baadhi wakipendekeza Zitto avuliwe nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu kwa maelezo kuwa anakwenda kinyume na taratibu za chama hicho na wengine wakipinga hatua hiyo kwa maelezo kuwa haina tija.
Mpaka saa moja usiku jana gazeti hili likienda mitamboni,  kikao hicho kilikuwa bado kikiendelea na suala hilo lililokuwa chini ya ajenda ya hali ya siasa nchini.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa chama hicho, Benson Kigaila aliahidi kuwa taarifa rasmi ya kikao hicho ingetolewa baadaye na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Tuhuma za Zitto
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwanzoni mwa Novemba mwaka huu aliingia katika malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, akituhumiwa na Lema kuwa anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho kutoka mashirika mbalimbali nchini.
Pia, aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutumia kofia yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kauli ambayo jana Kigaila aliitolea ufafanuzi na kueleza kuwa Chadema kimekaguliwa na hesabu zake tayari zipo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Hekaheka za jana
Mvutano wa jana ulianza baada ya Mbowe kufungua kikao hicho saa 4:00 asubuhi.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe, wakiwamo wabunge, walitaka Zitto avuliwe nafasi aliyonayo na kuwa mwanachama wa kawaida, huku wengine wakipinga hatua hiyo kwa maelezo kuwa Zitto hakuwepo katika kikao hicho na kwamba alipaswa kusikilizwa.
Credit:Mwananchi

No comments:

Post a Comment