![]() |
| Kamanda Massawe |
Na Gowdin Lyakurwa TANGA
Jeshi la
Polisi Mkoani Tanga linamtafuta Dereva wa Gari namba T765 AXT aina ya Mitsubishi
Fuso lililokuwa likitokea Korogwe kwenda katika kijiji cha Mgambo kwa
kusababisha ajali iliyo pelekea kifo cha Mtu mmoja.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Cosntantine Massawe
amesema kuwa tukio hilo limetokea Nov 21 mwaka huu majira ya saa 4:00 jioni
katika barabara ya Korogwe- ambapo gari hilo likiendeshwa na dereva ambaye
hajafahamika liliacha njia na akugonga mti ambao ulimuangukia mwendesha
baiskeli alietambulika kwa jina la Mohammed Ally (28)Mkazi wa Mgambo na
kufariki dunia hapo hapo.
Kamanda Massawe amesema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni uzembe wa Dereva wa Gari hilo ambaye alikimbilia kusikojulikana baada
ya tukio hilo.Mwili wa Mohammed umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe kwa
uchunguzi zaidi na Jeshi la Polisi linandelea na upelelezi ili kumbaini na kumkamata
Dereva huyo.
Wakati huohuo
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia Hassan Juma (23) mkaazi wa kata ya
kibirashi,Tarafa ya Mgera Wilaya ya Kilindi kwa kusababisha kifo cha Mtoto
Salehe Sufiani(5) kwa kumgonga na pikipiki.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga Costantine Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo
Nov 21 mwaka huu majira ya saa 4:00 jioni katika kata ya kibirashi,Tarafa ya
Mgera Wilaya ya Kilindi ambapo Hassani akiwa anaendesha pikipiki namba T 998
CCL alimgonga Mtoto Salehe Sufiani (5)mwanafunzi wa shule ya Kibirashi na
kufariki hapohapo.
Chanzo cha
ajali hiyo ni mwendokasi wa Pikipiki hiyo ambapo jeshi la Polisi
linamshilikilia Mtuhumiwa kwa ajili ya kumchukulia hatua za kisheria.Mwili wa
Mtoto huyo umekabidhiwa kwa ndugu zake baada ya kufanyiwa Uchunguzi.
Kufuatia matukio
hayo kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Costantine Massawe ametoa wito kwa watumiaji
wa Barabara kuwa makini na kuchukua taadhari wawapo barabarani hasa wakati wa Mwisho
wa Mwaka.

No comments:
Post a Comment