HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 16 November 2013

WAHAMIAJI HARAMU RAIA 22 WA ETHIOPIA WAKAMATWA DAR



 
Wahamiaji Haramu

RAIA 22 wa Ethiopia wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa  tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Ofisa Uhamiaji Mkoa, Grace Hokororo, alisema Wahabeshi hao walikamatwa juzi usiku katika maeneo ya Kinondoni wakiwa katika pagale ambamo walikuwa wamejificha.

Alisema baada ya wananchi kuwaona waliwatilia mashaka na ndipo walipotoa taarifa polisi ambao walifika na kuwakamata.
“Hii hali ilikuwa imepoa lakini hivi sasa naona tena wameibuka kwa kweli kazi ipo na hawa tunategemea kuwasafirisha na kuwarudisha kwao wakiwemo Wanyarwanda tisa,’’ alisema Hokororo.

Alisema wiki tatu zilizopota jumla ya wahamiaji 42 wakiwemo Wahabeshi, Wasomali na Wanyarwanda walisafirishwa na kurudishwa makwao.
Alisema pamoja na jitihada za idara hiyo kuwakamata raia hao, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi na magari, jambo alilosema limekuwa likikwamisha jitihada za idara hiyo katika kutekeleza majukumu yake.

“Watumishi wengi wamechukuliwa na NIDA na hapa nimebakiwa na wachache na magari pia ni tatizo tunaiomba serikali iliangalie na ione umuhimu wa kutuongezea watumishi ili tuweze kufanya kazi vizuri,” alisema.

No comments:

Post a Comment