![]() |
| BADRA MASOUD |
SHIRIKA la Umeme la Tanzania (TANESCO), limetangaza kuwapo kwa upungufu wa umeme katika mikoa yote inayotegemea gridi ya taifa kuanzia leo.
Mikoa itakayoathirika na tatizo hilo ni Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Morogoro, Singida, Mbeya, Manyara, Zanzibar, Shinyanga na Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa TANESCO, Badra Masoud, alisema upungufu huo wa umeme utadumu hadi Novemba 26 mwaka huu.
Alisema kila mkoa utakosa umeme kwa muda wa saa mbili kwa siku kwa nyakati tofauti.
Masoud alisema tatizo hilo linatokana na upungufu wa gesi kutoka katika kituo cha Songosongo kilichoko wilaya ya Kilwa, mkoa wa Lindi, unaosababishwa na matengenezo ya kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na kampuni ya Pan Afrika.
“Matengenezo ni muhimu hayaepukiki, lengo la matengenezo hayo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo,” alisema.


No comments:
Post a Comment