HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 16 November 2013

MAJANGILI YA TEMBO YAHUKUMIWA MIAKA 70 JELA



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha  miaka 70 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno manne ya tembo yenye thamani ya sh milioni 45.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Ntengwa, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.
 
TEMBO AKIWA AMEUWAWA

Waliohukumiwa kifungo hicho ni Gwabi Mayala (39)  mkazi wa kijiji cha Majimoto, wilaya ya Mlele, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30  jela na kulipa fidia ya sh milioni 45; na Mashaka Mabanga (33),  mkazi wa Sumbawanga, mkoani Rukwa na Adam Kalinzi (30), mkazi wa kijiji cha Majimoto, wamehukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka 20 jela.
Kabla ya hukumu hiyo, washtakiwa Mashaka na Adam walikiri kukamatwa na meno hayo ya tembo, lakini walidai meno hayo ni ya Mayala ambaye alikuwa amewaomba wamtafutie wateja.

Kwa upande wake, mshtakiwa Mayala aliiomba mahakama isikubaliane na maelezo ya washtakiwa wenzake kwa kuwa hayana ukweli.
Awali katika kesi hiyo, Mwanasheria wa Serikali, Fadhili Mwandoloma,  alidai washtakiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba 10  mwaka huu, saa 4:00 usiku katika kijiji cha Majimoto, wilayani Mlele.

Alidai siku ya tukio washtakiwa walikamatwa wakiwa na meno manne ya tembo yenye uzito wa kilo 16 wakiwa katika harakati ya kuyauza.

No comments:

Post a Comment