| Karia akizungumza katika ufunguzi wa michuano hiyo |
| Waamuzi wakianzisha mchezo |
TIMU ya Azam Fc inayoshiriki michuano ya vijana wenye
umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom leo imeanza
vibaya mashindano hayo baada ya kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga.
Azam ambao walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya tatu kupitia
kwa mshambuliaji Eric Haule baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Coastal Union, bao
ambalo lilidimu kwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kufanya mabadiliko, hali iliyofanya
mchezo kubadilika na kushambuliana kwa zamu lakini zamu hii Coastal waliizidi
Azam Fc kila sehemu.
Iliichukua Coastal Union dakika tano (daakika ya 50) kwenye kipindi cha
pili kusawazisha bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji Raizin Haji kwa njia ya
penati baada ya beki wa Azam Fc kunawa mpira eneo la hatari.
Dakika tano baadae (dakika ya 55) Raizin Haji aliifungia Coastal bao la
pili baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Azam hadi golikipa na kutia mpira
wavuni kirahisi na kuamsha nderemo na vifigo kwa mashabiki waliokuwa wamefurika
uwanjani hapo.
Baada ya matokeo hayo Azam walionekana kuchoka na kushindwa kuhimili
mashambulizi ya Coastal lakini shukrani kwa mlinda mlango wao Hamadi Juma kwani
alijitahidi kuokoa michomo mingi licha ya kufungwa hayo mabao mawili.
Awali akifungua mashindano hayo Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka
Nchini (TFF) Wales Karia alishukuru udhamini wa maji ya Uhai kwani umesaidia
kuibua vipaji na kusema TFF ina mikakati ya kuongeza mashindano mengi ya
kuhusisha umri ukiacha yale ya U-15 yanayodhaminiwa na Coca cola.
“Nashukuru udhamini wa maji ya Uhai kwani vijana wanatakiwa wacheze mara
kwa mara ili kusaidia kuinua vipaji ambavyo vitakuwa hazina kwa taifa hapo
baadae”, alisema Karia.
![]() |
| Kocha wa Coastal Yusuf Chiko |
| Wachzaji wa Coastal wkishangilia |

No comments:
Post a Comment