HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.
KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA
....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....
Pages
Sunday, 17 November 2013
CAMEROUN YACHAPA TUNISIA 4-1, HIYOOO BRAZIL 2014!
>>NI REKODI, NI MARA YA 6 FANAILI ZA KOMBE LA DUNIA!!
CAMEROUN leo huko Yaounde wameibonda Tunisia Bao 4-1 na kuwa Nchi ya 3 toka Afrika,kufuatia Jana Nigeria na Ivory Coast, kufuzu kwenda Brazil Mwakani kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Cameroon 4
-Pierre Webo Dakika ya 4
-Benjamin Moukandjo 30
-Jean Makoun 66 & 86
Tunisia 1
-Ahmed Akaichi 51
++++++++++++++++++++++++++++
Hii ni mara ya 6 kwa Cameroun kucheza Fainali za Kombe la Dunia na mara nyingine zikiwa Miaka ya 1982, 1990, 1994, 1998, 2002 na 2010 ambayo ni Rekodi kwa Afrika.
++++++++++++++++++++++++++++
AFRIKA
RATIBA/MATOKEO:
Marudiano:
Jumamosi Novemba 16
Nigeria 2 Ethiopia 0 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 4-1]
Senegal 1 Ivory Coast 1 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 2-4]
Jumapili Novemba 17
Cameroon 4 Tunisia 1 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 4-1]
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana [1-6]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]
**FAHAMU: Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia
++++++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi ya kwanza huko Tunis, Cameroun na Tunisia zilitoka Sare 0-0 lakini leo Cameroun walistahili kwa kila kitu ushindi wao kwa jinsi walivyotawala na kudhibiti Mechi hii huku Nahodha wao Samuel Eto’o leo akiwa mlishaji na mwongozaji mkuu.
Sasa Afrika imeshapata Timu 3 za kwenda Brazil na mbili za mwisho zitapatikana Jumanne kwenye Mechi mbili za mwisho kati ya Algeria na Burkina Faso na Egypt na Ghana.
VIKOSI VILIVYOANZA:
CAMEROON: Charles Itandje, Benoit Assou-Ekotto, Nicolas Nkoulou, Aurelien Chedjou, Benjamin Moudandjo, Alex Song, Enoy Eyong, Jean Makoun, Stephane Mbia, Samuel Eto'o, Pierre Webo
TUNISIA: Moez Ben Cherifia, Sameh Derbaly, Karim Haggui, Syam Ben Youssef, Fakhreddin Ben Youssef, Houcine Ragued, Yassine Chikhaoui, Wissem Ben Yahia, Yassin Mikari, Saber Khalifa, Amine Chermiti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment