| Rais Kikwete akisaini kitabu cha waombolezaji waliofika nyumbani kwa Mvungi Kibamba jijini Dar Es Salaam |
Tume ya
Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za kuusafirisha
mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki nchini Afrika Kusini
zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili nchini siku ya Ijumaa, Novemba
15, 2013.
Aidha, siku ya
Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika Kanisa Katoliki
la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi. Baada ya
misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku
hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16, 2013.
Dkt. Mvungi
alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya Millpark jijini
Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili ya uchunguzi na
matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa
baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili,
Novemba 3, 2013.
Wakati
huohuo, Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba hapo jana(Jumatano,
Novemba 13, 2013) wameungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt. Mvungi
eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu
na jamaa wa marehemu Dkt. Mvungi.
Mwisho.
Imetolewa
na:
Ndg.
Assaa A. Rashid,
Katibu,
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar
es Salaam
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu
Abdulrahaman Kinana amesikitishwa na taarifa ya kifo Cha Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea Jana katika Hospitali ya
Millpark nchini Afrika ya Kusini.
Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu
anawapa pole wanafamilia, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Warioba na Uongozi wa Chama Cha NCCR-Mageuzi. Hakika Taifa limepoteza Mtaalamu
wa Sheria, Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi ambacho mawazo yake
yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa hili.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali
pema peponi.
Imetolewa na:
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
13/11/2013
No comments:
Post a Comment