| Timu ya Polisi Jamii Wakati wa Mapumziko wakiwa pembeni ya Uwanja huo |
Michuano ya Massawe Cup inaendelea kutimua Vumbi katika Dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga na sasa imefikia hatua ya fainali ambayo itazikutanisha timu za Kiomoni Fc dhini ya Vijana Star mchezo utakao pigwa katika Uwanja huohuo wa Mkwakwani mnamo Nov 16.
Katika hatua ya nusu fainali timu ya Vijana Star iliitoa timu ya Vijana Kombezi kwa kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-0 yakifungwa na Shabani Adamu, Ramadhani Wambura .na Mbwana Hassani.
Kiomoni Fc wameitoa timu ya Polisi Jamii kwa mikwaju ya Penati 5-4 kufuatia suluhu ya bao 101 katika dakika 90.
Hata hivyo timu hizo zimejikuta katika wakati mgumu kwa kukosa sehemu nzuri ya kubadilishia nguo na kupikea mawaidha ya Walimu wao na kujikuta wakitumia maeneo ya Wazi ambayo hata hivyo yana Usumbufu kutoka kwa mashabiki.
| Wachezaji wea Kiomoni Fc wakiwa nje ya Uwanja wa Mkwakwani pamoja na kocha wao wakati wa Mapumziko |
No comments:
Post a Comment