| Kikosi Cha The Tanzanite |
Timu ya
Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 The Tanzanite imechaibanga Timu
ya Wenzao ya Taifa ya Msumbiji kwa Jumla ya mabao 15-1 baada ya kupata ushindi
mwingine mnono wa mabao 5-1 katika mchezo uliochezwa hii leo katika Dimba la
Zimpeto jijini Maputo nchini Msumbiji.
Mabao ya The
Tanzanite leo yamewekwa kimiani na Selda Boniface aliefunga matatu “hart trik”
Vumilia Maarifa na Dionosian Maarifa aliofunga bao 1 kila mmoja.
Timu hiyo ya
Msumbiji imetolewa kwa jumla ya magoli 15-1 baada ya kufungwa kipigo cha 10-0
walichokipata wakiwa ugenini nchini Tanzania wiki 2 zilizo pita na cha 5-1
walichokipata leo wakiwa nyumbani kwao nchini Msumbiji.
Kwa matokeo
hayo Tanzanite wanasubiri mshindi kati ya Botswana na Africa ya Kusini ambapo
wakishinda wataingia rasmi kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kombela Dunia
nchini CANADA.
No comments:
Post a Comment