RONALDO APIGA HETITRIKI, REAL
YAFUMUA 5-1!!
Cristiano
Ronaldo hapo jana amepata Hetitriki yake ya 23 kwa Real Madrid wakati Klabu yake
hiyoilipoitwanga Real Sociedad Bao 5-1 kwenye Mechi ya La Liga.
Ronaldo
ndie aliefunga Bao la kwanza kabla kumlisha Karim Benzema kufunga Bao la
Pili na kufuatia Penati aliyofunga Ronaldo Bao la 3 kwa Real.
++++++++++++++++++
MAGOLI:
Real
Madrid 5
-Ronaldo
Dakika ya 12, 26 (Penati), & 76
-Benzema
18
-Khedira
36
Real
Sociedad 1
-Griezmann
61
++++++++++++++++++
Gareth
Bale akamtengenezea Sami Khedira kupiga Bao la 4 na Real Sociedad wakapata
Bao lao moja Mfungaji akiwa Antoine Griezmann.
Ronaldo
alifunga Bao lake la 3 kwenye Mechi hii na la 5 kwa Real kwa frikiki safi.
Ushindi
huu umewafanya Real, walio Nafasi ya 3 na wakiwa wamecheza Mechi moja
zaidi, kufikisha Pointi 31 na mbele yao wapo Atletico Madrid wenye Pointi
33 na Barcelona Pointi 34.
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za
Bongo]
Ijumaa
Novemba 8
Granada
CF 3 Malaga CF 1
Osasuna
0 Almeria 1
Jumamosi
Novemba 9
Real
Madrid 5 CF Real Sociedad 1
2000
Getafe v Elche
2200
Athletic de Bilbao v Levante
0000
Celta de Vigo v Rayo Vallecano
Jumapili
Novemba 10
1400 RCD
Espanyol v Sevilla FC
1900
Valencia v Real Valladolid
2100
Villarreal v Atletico de Madrid
2300
Real Betis v FC Barcelona
LIGI KUU
ENGLAND
PENALTI TATA YAIOKOA CHELSEA,
LIVERPOOL YABAMIZA!
+++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za
Bongo]
Jumamosi
Novemba 9
Aston
Villa 2 Cardiff 0
Chelsea
2 West Brom 2
Crystal
Palace 0 Everton 0
Liverpool
4 Fulham 0
Southampton
4 Hull City 1
20:30
Norwich v West Ham
++++++++++++++++++++++++
ASTON
VILLA 2 CARDIFF 0
Frikiki
ya Leandro Bacuna katika Dakika ya 76 na kichwa cha Dakika ya 84 cha Libor
Kozak leo kimemaliza Masaa 7 na Nusu bila kutingisha wavu na kuwapa Aston
Villa ushindi wa Bao 2-0 Uwanjani kwao Villa Park walipoifunga Cardiff
City.
VIKOSI:
Aston
Villa: Guzan,
Bacuna, Vlaar, Clark, Baker, El Ahmadi, Westwood, Sylla, Tonev, Benteke,
Kozak
Cardiff:
Marshall,
Taylor, Caulker, Turner, Whittingham, Medel, Odemwingie, Gunnarsson, Cowie,
Theophile-Catherine, Bellamy.
++++++++++++++++++++++++
CHELSEA
2 WEST BROM 2
Leo
Uwanjani kwao Stamford Bridge, Chelsea itabidi wamshukuru Refa Andre
Marriner kwa kuwaokoa toka kwenye kipigo baada ya kuwapa Penati tata katika
Dakika ya 93 wakati West Brom wanaongoza Bao 2-1.
Penati
hiyo ilitolewa na Refa huyo baada ya Mchezaji wa Chelsea Ramires kuanguka
baada kugongana na Steven Reid na Penati hiyo kufungwa na Eden Hazard.
 |
| Samuel Etoo |
Chelsea
ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 45 kwa Bao la Samuel Eto'o
lakini Kipindi cha Pili West Brom wakafunga Bao mbili kupitia Shane Long
Dakika ya 60 na Stephane Sessegnon Dakika ya 68.
Baada
Dakika 90 kwisha Bango likaonyesha Dakika 4 za nyongeza na ndipo Dakika ya
93 ikaja Penati tata iliyolinda Rekodi ya Jose Mourinho ya kutofungwa
Nyumbani kwenye Ligi.
VIKOSI:
Chelsea:
Cech;
Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Ramires, Lampard; Hazard, Oscar,
Willian; Eto'o
West
Brom: Myhill;
Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell; Yacob, Mulumbu; Amalfitano, Sessegnon,
Brunt; Long
++++++++++++++++++++++++
CRYSTAL
PALACE 0 EVERTON 0
Crystal
Palace leo wamepata Pointi yao ya kwanza katika Mechi 8 za Ligi walipotoka
Sare ya 0-0 na Everton.
VIKOSI:
Crystal
Palace: Speroni,
Ward, Gabbidon, Delaney, Moxey, Jedinak, Dikgacoi, Bannan, Thomas, Bolasie,
Chamakh
Everton:
Howard,
Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Osman,
Pienaar, Lukaku
++++++++++++++++++++++++
LIVERPOOL
4 FULHAM 0
Wakiwa
kwao Anfield, Liverpool wameifumua Fulham Bao 4-0 kwa Bao za Fernando
Amorebieta, kwa kujifunga mwenyewe, Martin Skrtel na Bao mbili za
Luis Suárez.
Ushindi
huu umeifanya Liverpool wakamate Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya
Arsenal.
VIKOSI:
Liverpool:
Mignolet,
Johnson, Skrtel, Agger, Cissokho, Lucas, Gerrard, Henderson, Coutinho,
Suarez, Sturridge
Fulham: Stekelenburg, Zverotic,
Senderos, Amorebieta, Richardson, Dejagah, Parker, Sidwell, Kacaniklic,
Kasami, Berbatov
++++++++++++++++++++++++
SOUTHAMPTON
4 HULL 1
Southampton
leo wameendeleza matokeo mazuri kwa Timu yao Msimu huu kwa kuichapa Hull
City Bao 4-1.
Bao za
Southamton zilifungwa na Morgan Schneiderlin, Rickie Lambert, kwa Penati,
Adam Lallana na Steven Davis.
Bao la
Hull City lilifungwa na Yannick Sagbo.
VIKOSI:
Southampton:
Boruc,
Clyne, Fonte, Lovren, Shaw, Wanyama, Schneiderlin, Ward-Prowse, Lallana,
Rodriguez, Lambert
Hull
City: Harper,
Rosenior, Figueroa, Davies, McShane, Elmohamady, Boyd, Meyler, Huddlestone,
Livermore, Sagbo
++++++++++++++++++++++++
RATIBA
[Saa za
Bongo]
Jumapili
Novemba 10
15:00
Tottenham v Newcastle
17:05
Sunderland v Man City
19:10
Man United v Arsenal
19:10
Swansea v Stoke
++++++++++++++++++++++++
SERIE A: LEO JUMAPILI NI JUVENTUS
v NAPOLI!!
>>VINARA
AS ROMA KUCHEZA NA TIMU YA MKIANI SASSUOLO CALCIO!
Jumapili
huko Italy kwenye SERIE A, Mabingwa wa Italy Juventus watawakaribisha
Napoli kwenye pambano ambalo zinazikutanisha zilizo Nafasi za Pili na za
Tatu kwenye Ligi, zote zikiwa na Pointi sawa, Pointi 28, ambazo ni 3 nyuma
ya Vinara AS Roma.
Napoli
wanakamata Nafasi ya Pili mbele ya Juventus kwa sababu ya ubora wa Magoli.
++++++++++++++++++++
SERIE A
MSIMAMO-Timu
za Juu:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
AS
Roma
|
11
|
10
|
1
|
0
|
25
|
2
|
23
|
31
|
2
|
SSC
Napoli
|
11
|
9
|
1
|
1
|
24
|
8
|
16
|
28
|
3
|
Juventus
FC
|
11
|
9
|
1
|
1
|
23
|
10
|
13
|
28
|
4
|
Inter
Milan
|
11
|
6
|
4
|
1
|
27
|
12
|
15
|
22
|
5
|
Hellas
Verona
|
11
|
7
|
1
|
3
|
22
|
17
|
5
|
22
|
6
|
ACF
Fiorentina
|
11
|
6
|
3
|
2
|
22
|
13
|
9
|
21
|
++++++++++++++++++++
Wakati
pambano hilo kali likichezwa Juventus Stadium, Vinara AS Roma watakuwa
Nyumbani kucheza na US Sassuolo Calcio ambao wako Nafasi ya 3 toka mkiani
wakiwa na Pointi 9 tu.
Juve na
Napoli zinatinga kwenye Mechi hii zikitoka kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI
ambako Juve walitoka Sare ya 2-2 na Real Madrid na Napoli kuifunga
Marseille Ba0 3-2.
Kwenye
Serie A, Napoli, chini ya Kocha Rafael Benitez, na Juve, chini ya Antonio
Conte, zote zipo kwenye wimbi la kushinda Mechi 3 mfululizo.
Juve
watatinga kwenye mtanange huu na Napoli bila ya Stephan Lichtsteiner, Mirko
Vucinic na Simone Pepe ambao ni majeruhi.
Napoli,
ambao watakuwa na Kikosi kamili, watawategemea zaidi Jose Callejon, Marek
Hamsik na Gonzalo Higuaian kuwapa ushindi lakini huko Turin ambako
wamekutana mara 67 na Juve, Napoli wameshinda mara 7 tu na kufungwa mara 40
kikiwemo kipigo cha 2-0 Msimu uliopita.
VIKOSI
VINATARAJIWA:
Juventus:
Buffon;
Barzagli, Bonucci, Chiellini; Isla, Vidal, Pirlo, Pogba, Asamoah;
Quagliarella, Tevez
Napoli: Reina; Maggio, Fernandez, Cannavaro,
Armero; Inler, Behrami; Callejon, Hamsik, Mertens; Higuain
SERIE A
RATIBA:
[Saa za
Bongo]
Jumamosi
Novemba 9
2000
Calcio Catania v Udinese Calci
2245
Inter Milan v AS Livorno Calcio
Jumapili
Novemba 10
1430
Genoa v Hellas Verona FC
1700
Atalanta v Bologna FC
1700 AC
Chievo Verona v AC Milan
1700
Parma v SS Lazio
1700 AS
Roma v US Sassuolo Calcio
1700
Cagliari Calcio v Torino FC
2245
Juventus v SSC Napoli
2245 ACF
Fiorentina v UC Sampdoria
NANI BINGWA AFRIKA, AL AHLY
AU ORLANDO PIRATES??
JUMAPILI
Usiku huko Cairo Nchini Egypt Klabu Bingwa ya Afrika itapatikana baada ya
Mechi ya Marudiano ya Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI kati ya Mabingwa
Watetezi Al Ahly ya Egypt na Orlando Pirates ya Afrika Kusini huku Al Ahly
wakiwa na hazina ya Bao la Ugenini kwani Timu hizi zilitoka Sare ya Bo 1-1
huko Johannesburg Wiki iliyopita.
Katika
Mechi hiyo ya kwanza Al Ahly walitangulia kufunga kwa Bao la frikiki ya
Mkongwe Mohamed Aboutrika katika Dakika ya 14 na Pirates kusawazisha kwa
Bao la mwishoni la Dakika za Majeruhi la Thabo Matlaba.
 |
| Thabo Matlaba |
Timu
hizi pia zilikuwa kwenye Kundi moja kwenye Mashindano haya na Pirates
kuifunga Al Ahly 3-0 huko Egypt kwenye Mechi ambayo walidai kipigo hicho ni
kwa sababu walikuwa kwenye Mfungo wa Ramadhani.
Katika
Marudiano huko Johannesburg, Pirates na Al Ahly zilitoka 0-0 na zote hizi
kufuzu kuingia Nusu Fainali.
Kwenye
Nusu Fainali, Pirates waliibwaga Esperance ya Tunisia kwa Bao la Ugenini
baada kutoka 0-0 huko Johannesburg na 1-1 huko Tunis.
Nao Al
Ahly walitoka 1-1 na Coton Sport ya Cameroun katika Mechi zao zote mbili na
Al Ahly kutinga Fainali kwa Mikwaju ya Penati 7-6.
Wakati
Orlando Pirates wametwaa CAF CHAMPIONZ LIGI mara 1 tu, Mwaka 1995, Al Ahly
washabeba Ubingwa huu mara 7.
Mechi
hii ya Marudiano itaanza Saa 1 Usiku kwa Saa za Bongo na kurushwa moja kwa
moja na Kituo cha TV cha SuperSport.
|
|
No comments:
Post a Comment