Naibu waziri wa mawasiliano nchini Ghana Victoria Hammah
ameachishwa kazi baada ya kunukuliwa akisema kuwa atasalia katika siasa hadi
atakapo pata fedha kiasi cha dola milioni moja.
![]() |
| Victoria Hammah |
Mwandishi wa BBC mjini Accra anasema Bi Hammah alikuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa rais John Mahama mwaka jana.
Baada ya uteuzi wake baadhi ya wadadisi walionya kuwa ana umri mdogo sana kuweza kuhudumu katika serikali.Mwezi Agosti alinukuliwa akisema kuwa kuna shinikizo za kumtaka aibe fedha za umma kwa kuwa watu hudhani kwamba yeye ni tajiri kwa sababu ya wadhifa wake wa uwaziri.
Katika kanda hiyo alisikika akisema kuwa hatatoka katika siasa hadi atakapopata dola milioni moja.Pia alisikika akimkosoa waziri mwenzake akisema hana akili,ana sura mbaya na anapenda sana kujigamba na kuwafokea watu.

No comments:
Post a Comment