Makubaliano
kusainiwa Jumatatu Kampala
Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo itatia saini makubaliano
ya amani siku ya Jumatatu na kundi la
waasi la M23 baada ya kundi hilo
kuweka silaha zao chini wiki hii kufuatia
kushindwa katika mapambano.
Waziri wa mambo
ya kigeni wa Kongo, Raymond Tshabanda, ameliambia
shirika la habari la Reuters leo kuwa
imeamuliwa siku moja baada ya kundi
la M23 kutangaza kuachana na uasi wao
kuwa serikali itawapa siku tano kabla ya
kutia saini.
Akiwa katika ziara nchini Ufaransa,
Tshabanda amesema kuwa utiaji saini ni
muhimu kwa sababu unalenga kuwaingiza wapiganaji
wa M23 katika makambi ya jeshi la
nchi hiyo na kulivunja kabisa kundi hilo
pamoja na kutatua matatizo mengine.


No comments:
Post a Comment