Huku
ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa imekamilisha mzunguko wake wa kwanza hii
leo,timu ya Azam FC ya Dar es Salaam imetangaza kusitisha mkataba na kocha wake
mkuu Stewart Hall wa Uingereza kwa kile kilichoelezwa kama makubaliano ya
pamoja.
![]() |
Stewart Hall |
Klabu ya Azam FC inayoinukia kwa ubora wa miundo mbinu huku ikiendeshwa kisasa kwa mipango inayoeleweka kinyume na klabu nyingi nchini Tanzania imekuwa ikifanya vema chini ya mwalimu huyo ambapo msimu uliopita aliiwezesha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kushika nafasi ya Pili katika Ligi kuu msimu uliopita.
Klabu hiyo inao wachezaji kadhaa wa Kulipwa kutoka nchi za Ivory Coast, Kenya na Uganda. Kuachia ngazi kwa kocha huyo kunaelezwa kuwa kumekuwa kwa mkakati ili kusiathiri mwenendo wa timu hususan wakati ligi ikiendelea na sasa kutaiwezesha Azam FC Kutafuta kocha mwingine hususan wakati huu ambapo ligi imefikia mapumziko.

No comments:
Post a Comment