![]() |
| Mzee Kinesi |
MWENYEKITI aliyesimamishwa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage atarejea nchini Ijumaa na kulakiwa na mamia ya wanachama na ataitisha Mkutano Mkuu, ambao utafanyika Jumapili hii.
Na katika Mkutano huo, Rage amepanga kuwasimamisha Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji na baada ya hapo atasafiri kwenda nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliobaki Simba SC ni Joseph Itang’are ‘Kinesi’, Said Pamba, Ibrahim Masoud ‘Maestro’, Swedi Nkwabi na Zacharia Hans Poppe.
Baada ya hapo, Rage ataitisha Mkutano Mkuu wa dharula Jumapili na siku hiyo atawasimamisha Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji.
Rage ambaye kwa sasa yuko nchini Sudan kwa shughuli
zake za kisiasa.
Rage anatuhumiwa kuchukua maamuzi mazito ya klabu
bila kuwashirikisha wenzake na mengi yamekuwa yakiiweka klabu matatani. Pia,
anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za klabu na kukwamisha mambo mengi ya
kimaendeleo ndani ya klabu, ikiwemo mabadiliko ya Katiba.
Baada ya kumsimamisha Rage, Kamati ya Utendaji pia ilimteua Joseph Itang’are ‘Kinesi’ kukaimu Uenyekiti wa klabu hadi hapo Mkutano Mkuu utakapofanyika.
Kinesi pia alikuwa anakaimu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu, iliyoachwa wazi na Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyejiuzulu mapema mwaka huu, ambaye sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Pamoja na kumsimamisha Rage, Kamati ya Utendaji pia imewasimamisha makocha wa kikosi cha kwanza, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ na Msaidizi wake, Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’.
Kamati imeamua kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha wa timu ya vijana, Simba B, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ ambaye atakuwa pia Msaidizi wa kocha Mkuu mpya wa kigeni, atakayetambulishwa Desemba 1, mwaka huu.

No comments:
Post a Comment