
DABI
YA MERSEYSIDE: AGGER WA LIVERPOOL AKIRI EVERTON NGUMU!
BEKI wa Liverpool Daniel Agger
anatarajia Dabi ya Merseyside, ile Mechi kati ya Klabu za Jiji la Liverpool
Everton na Liverpool, Wikiendi hii itakuwa ngumu mno kama ilivyo kawaida.
Jumamosi, Uwanjani Goodison Park,
Everton itaikaribisha Liverpool katika Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu
England Wikiendi hii ambayo inarejea kilingeni baada ya Wiki mbili kupisha
Mechi za Kimataifa.
++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi 23 Novemba
[Saa za Bongo]
1545 Everton v Liverpool
1800 Arsenal v Southampton
1800 Fulham v Swansea City
1800 Hull City v Crystal Palace
1800 Newcastle United v Norwich City
1800 Stoke City v Sunderland
2030 West Ham United v Chelsea
++++++++++++++++++++
Agger amekiri kuwa Msimu huu Everton,
chini ya Meneja mpya Roberto Martinez, imekuwa kali mno.
Agger amesema: “Ni juu ya Pointi 3 tu
na tunatumaini tutazipata. Siku zote Dabi hii ni ngumu mno. Everton Msimu huu
wameanza vizuri, wana Meneja mpya na staili tofauti kidogo.”
Pia Agger alifafanua kuwa licha ya
Liverpool kuwa Nafasi ya Pili ni mapema mno kusema nani atashinda mbio za
Ubingwa.
Liverpool wako Pointi 2 nyuma ya Vinara
Arsenal na Everton wako Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Liverpool.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili 24 Novemba
1630 Manchester City v Tottenham
Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United
Jumatatu 25 Novemba
2300 West Bromwich Albion v Aston Villa
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
|
NA
|
TIMU
|
P
|
GD
|
PTS
|
|
1
|
Arsenal
|
11
|
12
|
25
|
|
2
|
Liverpool
|
11
|
11
|
23
|
|
3
|
Southampton
|
11
|
10
|
22
|
|
4
|
Chelsea
|
11
|
8
|
21
|
|
5
|
Man Utd
|
11
|
5
|
20
|
|
6
|
Everton
|
11
|
4
|
20
|
|
7
|
Tottenham
|
11
|
3
|
20
|
|
8
|
Man City
|
11
|
16
|
19
|
|
9
|
Newcastle
|
11
|
-1
|
17
|
|
10
|
West Brom
|
11
|
0
|
14
|
|
11
|
Aston Villa
|
11
|
-1
|
14
|
|
12
|
Hull
|
11
|
-5
|
14
|
|
13
|
Swansea
|
11
|
0
|
12
|
|
14
|
Cardiff
|
11
|
-6
|
12
|
|
15
|
Norwich
|
11
|
-12
|
11
|
|
16
|
West Ham
|
11
|
-2
|
10
|
|
17
|
Stoke
|
11
|
-4
|
10
|
|
18
|
Fulham
|
11
|
-9
|
10
|
|
19
|
Sunderland
|
11
|
-14
|
7
|
|
20
|
Crystal Palace
|
11
|
-15
|
4
|
BARCELONA
YATHIBITISHA VALDES NJE HADI 2014
KIPA wa Barcelona, Victor Valdez,
anakabiliwa na muda mrefu nje ya Uwanja baada kuumia kwenye Mechi ya Timu ya Taifa
ya Spain Jumanne walipofungwa 1-0 na Afrika Kusini.
Katika Mechi hiyo iliyochezwa Nchini
Afrika Kusini, Valdez, mwenye Miaka 31, alimbadili Iker Casillas wa Real Madrid
wakati wa Haftaimu lakini yeye alidumu Dakika 25 tu baada kuumia na nafasi yake
kuchukuliwa na Kipa wa Liverpool, Pepe Reina, ambae yuko Napoli kwa Mkopo.
Madaktari wa Timu ya Spain walisema
Kipa huyo amechanika Musuli ya nyuma ya Mguu na atakuwa nje kwa Wiki 4 lakini
baada ya uchunguzi wa kina hii leo imethibitika kuwa atakuwa nje kwa muda mrefu
zaidi.
Hali hiyo imethibitishwa hii leo na
Taarifa rasmi ya Klabu ya Barcelona kwenye Tovuti yao ambayo imesema atakuwa
nje kwa muda usiopungua Wiki 6.
Pigo hili linafuatia lile la Klabu hiyo
kumkosa Nyota wao mkubwa Lionel Messi ambae nae ni majeruhi na atakuwa nje kwa
Wiki 6 hadi 8.
Valdez, ambae Msimu huu ameshaidakia
Barca Mechi 19, atazikosa Mechi za Timu yake za UEFA CHAMPIONZ LIGI za Kundi
lao dhidi ya Ajax na Celtic na Mechi za La Liga na Granada, Athletic Bilbao na
Villarreal.
Kuumia kwa Valdez ambae Mkataba wake
unamalizika Mwezi Juni na mwenyewe alishasema anaondoka kutaifanya Barca kusaka
Kipa wa kudumu haraka.
LA LIGA
RATIBA
[Saa za Bongo]
Ijumaa Novemba 22
2300 Real Valladolid v Osasuna
Jumamosi Novemba 23
1800 FC Barcelona v Granada CF
2000 Real Sociedad v Celta de
Vigo
2200 UD Almeria v Real Madrid CF
0000 Atletico de Madrid v Getafe
CF
Jumapili Novemba 24
1400 Levante v Villarreal CF
1900 Rayo Vallecano v RCD
Espanyol
2100 Elche CF v Valencia
2300 Sevilla FC v Real Betis
0000 Malaga CF v Athletic de Bilbao
No comments:
Post a Comment