![]() |
| Ronaldo |
FIFA imeongeza muda wa upigaji Kura kwa
ajili ya kuchagua Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2013 ambae atashinda Tuzo ya
Ballon d'Or na hali hii, Wachunguzi wamesema, itaongeza nafasi ya Cristiano
Ronaldo kutwaa Tuzo hiyo baada kuonyesha uhodari mkubwa ulioifanya Nchi yake
Portugal ifuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani.
Upigaji Kura sasa utakuwa wazi hadi
Ijumaa Novemba 29 wakati ulitakiwa kufungwa Novemba 15 na uongezwaji huu
umedaiwa na FIFA kuwa ni kwa sababu Wapigaji Kura wengi walishindwa kuwasilisha
Kura zao kwa wakati.
Ronaldo, ambae alitwaa Tuzo ya hii
Mwaka 2008, Jummane Usiku alipiga Bao zote 3 wakati Portugal inaifunga Sweden
3-2 huko Stockholm na kutua Brazil kwenye Kombe la Dunia.
Lionel Messi ametwaa Tuzo hii kwa Miaka
minne iliyopita.
Mshindi wa Ballon d'Or anachaguliwa kwa
Kura toka kwa Makocha wa Timu za Taifa na Manahodha wao pamoja na Mwanahabari
mmoja kutoka kila Nchi Wanachama wa FIFA ambapo kuna Wanachama 209.
Awali Dirisha la Upigaji Kura lilikuwa
ni kati ya Oktoba 28 hadi Novemba 15.
Washindi watatajwa Januari 13 Mjini
Zurich.
WAGOMBEA- Ballon
d'Or: Gareth Bale (Real Madrid), Edinson
Cavani (Paris St-Germain), Radamel Falcao (Monaco), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan
Ibrahimovic (Paris St-Germain), Andres Iniesta (Barcelona), Philipp Lahm
(Bayern Munich), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund), Lionel Messi
(Barcelona), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich),
Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (Juventus), Franck
Ribery (Bayern Munich), Arjen Robben (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Real
Madrid), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Luis Suarez (Liverpool),
Thiago Silva (Paris St-Germain), Yaya Toure (Manchester City), Robin Van Persie
(Manchester United), Xavi (Barcelona).
WAGOMBEA- Kocha Bora: Carlo Ancelotti (Real Madrid CF), Rafael BenÃtez (Napoli),
Antonio Conte (Juventus), Vicente Del Bosque (Spain), Sir Alex Ferguson
(Manchester United's former coach), Jupp Heynckes (Bayern Munich's former
coach), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe
Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal).

No comments:
Post a Comment