![]() |
| Rage |
Jana uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza kumsimamisha mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
Maamuzi
hayo yalitokana na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hapo juzi,
Hizi
ni Miongoni mwa sababu zilizotolewa kwenye mkutano wa waandishi wa habari
zilizopelekea kusimamishwa kwa Mheshimiwa Rage.
Mkataba na AZAM TV
Rage
alisaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya kipindi ya cha Simba TV bila
kuishirikisha kamati ya utendaji.
Wakati
Rage anasaini mkataba na Azam TV tayari klabu ya Simba ilikuwa kwenye
mazungumzo ya mwisho mwisho kuingia mkataba na kampuni ya ZUKU kwa ajili
kipindi cha Simba TV uliokuwa na thamani ya dola za kimarekani 300,000 kwa
mwaka.
Kampuni
ya ZUKU ilipokuwa kwenye majadiliano na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga
jijini Nairobi, kwenye mkutano huo Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa kamati ya
utendaji Joseph Itang’are maarufu kama mzee Kinesi pamoja na mwanachama Evans
Aveva wakati Yanga iliwakilishwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga na Francis
Kifukwe,viongozi hao Simba Ghafla walisikia Rage kasaini mkataba na Azam TV kwa
ajili ya Simba TV.
Sakata la uhamisho wa
Emmaanuel Okwi.
Mheshimiwa
Rage ndiye aliyesimamia uhamisho wa mchezaji Okwi on CREDIT bila kuishirikisha
kamati ya utendaji,matokeo yake klabu hiyo mpaka leo imeshindwa kupata pesa ya
uhamisho wa mchezaji huyo.
Kutoitisha vikao vya kamati ya
utendaji.
Sababu
nyingine iliyoelezwa ni kitendo chake cha kushindwa kuitisha vikao vya kamati
ya utendaji, Kuendesha klabu na kufanya maamuzi binafsi bila ya kushirikisha
kamati hiyo ya utendaji ambayo ilichaguliwa na wanachama
Strategic plan ( Mpango
mkakati )
Hivi
karibuni klabu ya Simba ilizindua mchakato wa kutengeneza mpango mkakati
(Strategic Plan) lakini cha kushangaza mwenyekiti amekuwa hataki kuona mpango
huo ukifanikiwa.
Mkutano mkuu wa katiba
Kushindwa
kuitisha mkutano wa marekebisho ya katiba,kuchukua maamuzi binafsi ya
kuhairisha mkutano maalumu wa katiba uliotakiwa kufanyika Novemba, mwaka huu.

No comments:
Post a Comment