![]() |
| Rage |
Kuhusu Rage
Aliyekuwa
akikaimu nafasi ya Umakamu uenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi
sasa ndiye mwenyekiti mpya Simba.
Itang’are
alikuwa akikaiumu nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Kaburu aliyeamua kuachia
ngazi.Sasa ndiye atakuwa mwenyekiti mpya wa Simba, saa chache tu baada ya
mwenyekiti, Ismail Aden Rage kusimamishwa.
Mmoja
ya wajumbe wa kamati ya utendaji, Swed Nkwabi yeye ameteuliwa kuwa kaimu makamu
mwenyekiti.
![]() |
| Mzee Kinesi (kushoto)akiwa na Julio(katikati) na Kibaden(kulia) |
KUHUSU KIBADEN
Baada ya kuwatimua makocha wake,
Abdallah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’, Simba sasa
imemchukua kocha Zdravko Logarusic
raia wa Croatia.
Tayari Simba imemaliza mazungumza na kocha huyo na
anatarajia kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kusaini mkataba na mara moja
kuanza kazi.
Kabla ya hapo, Logarusic alikuwa kocha wa Gor Mahia
ya Kenya aliyoifundisha kwa misimu miwili akisha nafasi ya pili.
Msimu huu ulikuwa wa mwisho, lakini aliondoka
katikati na nafasi yake kuchukuliwa na Bobby Williamson ambaye baadhi ya vyombo
vya habari viliripoti anajiunga na Simba, kitu ambacho hakikuwa sahihi.
Baadaye Bobby alikanusha kuwa amefanya mazungumzo
na Simba na ataendelea kubaki Kenya.
![]() |
| Selemani Matola |
KUHUSU JULIO
SULEIMAN Abdallah Matola sasa anakuwa Kaimu Kocha
wa Simba SC baada ya makocha wote, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’
na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kusimamishwa.
Matola ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Simba B, atakuwa Kocha Msaidizi wa kocha mpya wa kigeni, atakayetambulishwa Desemba 1, mwaka huu.
Kaimu
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ amewaambia Waandishi
wa Habari leo mchana makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi kwamba, pamoja na
kuwasimamisha makocha hao kwa kutoridhishwa na uwezo wao, pia wamemsimamisha
Mwenyekiti, Alhaj Ismail Aden Rage kwa madai hawana imani naye.
Kinesi alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika jana Dar es Salaam.
Kinesi amesema sasa yeye ndiye atakaimu Nafasi ya Uenyekiti wa klabu hadi hapo Mkutano Mkuu utakapofanyika.
Ikumbukwe Kinesi alichaguliwa kama Mjumbe tu wa Kamati ya Utendaji na Makamu Mwenyekiti ni nafasi ambayo anakaimu baada ya kujiuzulu kwa Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
Hata hivyo, Rage hakuwepo kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji jana na Kinesi alipoulizwa alisema kiongozi huyo yupo safarini.



No comments:
Post a Comment