HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 13 November 2013

MARUFUKU KUOA MWANAFUNZI HANDENI “WALIO HUSIKA WANASWA”


Muhingo Rweyemamu

ONYO hilo limetolewa kwa viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Handeni watakaojihusisha na kushiriki kuwaozesha wasichana walioko shuleni ya kuwa yeyote atakae bainika amefanya hivyo adhabu kali itachukuliwa juu yake kutokana na wimbi la kuwaozesha wanafunzi wa kike wilayani humo.

Onyo hilo limetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu kwa kusema kuwa hataweza kuvumilia baadhi ya viongozi kushiriki kuwaachisha wasichana shule na kuwatafutia wanaume waolewe kwa kusema kuwa mwanafunzi sio mke aachwe asome kwanza ili wajikomboe kimaisha.
Alisema kuwa kwa kuanza zoezi hilo tayari mtendaji wa kijiji cha Pozo ameshakamatwa kwa kosa la kushiriki kuwezesha kuolewa kwa mwanafunzi Sikujua Mganga mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Pozo ambapo mtendaji huyo alishiriki mchakato mzima wa mwanafunzi huyo hadi kumsafirisha na kumpeleka Dar Es Salaam.

“Kiongozi yeyote wa halmashauri ya wilaya ya Handeni akigundulika amehusika na kuozesha mwanafunzi adhabu kali juu yake lazima ipite,inasemekana kuna wakuu wa shule,viongozi wa dini na baadhi ya viongozi wengine wanahusika katika hili kwakweli siwezi kuvumilia nikikugundua siwezi kukuacha naanza na huyu mtendaji wa kijiji cha Pozo wengine mtafuata”alisema Rweyemamu.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka pia viongozi wa dini kuzingatia sheria za nchi kwa kutowafungisha ndoa watu ambao wanawasiwasi nao na iwapo watabaini mhusika ni mwanafunzi watoe taarifa haraka katika vyombo husika ili mhusika akamatwa huku akimuagiza afisa elimu wa shule za msingi kufuatilia suala hilo.

Aidha alizitaja shule ambazo zinaongoza kwa utoro wilayani humo kuwa ni shule ya msingi Mazingara,Kweditiribe na Pozo ambapo mkakati wa kuitisha mkutano wa wazazi unafanyika ili kuweza kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu kwa watoto wao.

Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya inakuja baada ya kugundua kuwa idadi ya wanafunzi watoro katika shule za msingi imeongezeka zaidi na kubainika kuwa wengi wa wanafunzi hao niwakike na imebainnika kuwa wameozeshwa.Wilaya hiyo iliathirika zaidi mwaka jana kwa tatizo la mimba ambapo ilikuwa ni asilimia 11 lakini kwasasa ni asilimia 0.1 na kumezuka suala la kuwaozesha tena wanafunzi.

No comments:

Post a Comment