Na Godwin Lyakurwa
TANGA
Jeshi
la Polisi Mkoani Tanga linawatafuta watu
wanne kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ujambazi wa kutumia silaha katika eneo
la Kange Kata ya Maweni jjini Tanga.
![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Costantin Massawe(picha na Maktaba) |
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Afisa Upelelezi Mkoa wa Tanga Aziz Kimata ameeleza kuwa
tukio hilo lilitokea mnamo siku ya Jumapili Nov 16/ 2013 mnamo majira ya saa 5:15 Usiku ambapo majambazi hao wanne
mmoja akiwa na bastola walivamia baa maarufu iliyoko maeneo hayo iitwayo Bongo
Pub na kupora Sh 550000/=,Tv ndogo na Vinywaji vyote mali ya mmiliki wa Baa
hiyo na kisha kutoweka kusiko julikana.
Hata
hivyo hakuna aliye jeruhiwa katika tukio hilo ambapo majambazi hao walifyatua
risasi hewani ili kuwatishia wananchi
waliokuwa jirani na eneo hilo.
Aidha
Eng Kimati ambaye ni Afisa Upelelezi Mkoa ametoa wito kwa wakaazi wa mkoa wa
Tanga na vitongoji vyake kutoa taarifa za uhalifu mapema hasa kabla haujatokea
iwapo watahisi mienendo isiyo salama kwa baadhi ya watu ili kuweza kudhibiti
uhalifu hasa katika kipindi hiki cha mwishi wa Mwaka.
Afisa
huyo ameeleza kuwa hakuna aliekamatwa
kuhusiana na tukio hilo la Ujambazi na Upelelezi ili kuwabaini watu hao
unaendelea.

No comments:
Post a Comment