HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 17 November 2013

*BREAKING NEWS* SIMBA YANZA USAJILI KWA MBWEMBE "YANASA WAWILI KWA MPIGO"



Awadh Juma Issa (Kushoto)Ally Baru ally(kulia) wakiwa na Rage (Katikati)Picha na Bin Zubeiry
Wekundu wa Msimbazi "SIMBA SC" imesajili wachezaji wawili kwa mpigo leo hii, kiungo mchezeshaji Awadh Juma Issa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro na Ally Badru Ally kutoka Canal Suez ya Ligi Kuu ya nchini Misri.
Wachezaji hao wawili wa timu ya soka ya taifa ya Zanzibar wamesaini adhuhuri ya leo, nyumbani kwa Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, Mtaa wa Samora, jijini Dar es Salaam.

Wachezaji hao walitua kwa ndege maalum na mchana wakaenda kusaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja na baada ya hapo, wakarejea kwenye kambi ya Zanzibar Heroes inayojiandaa na michuano ya CECAFA Challenge.

Akizungumza baada ya kuwasajili wachezaji hao, Rage alisema kwamba usajili huo umetokana na mapendekezo ya benchi la Ufundi la Simba SC.
“Ni wachezaji wazuri, ambao tunawajua vizuri na tumekuwa tukiwafuatilia kwa muda mrefu na tuna imani nao sana kwamba watakuja kuisaidia timu yetu,”alisema Rage.

Kwa upande wake, Ally Badru alisema kwamba amefurahi sana kusaini Simba SC na anaamini nyota yake itang’ara huko. “Simba SC ni timu kubwa, maarufu, naamini kabisa hapa nitafanya vizuri, kikubwa tu naomba sapoti ya mashabiki wote,”alisema.
Kuhusu klabu yake ya Misri aliyoichezea tangu mwaka 2010, Badru alisema kwamba imemruhusu kuondoka ingawa alikuwa ana miaka miwili zaidi katika Mkataba wake na klabu hiyo. 
Juma ambaye ameichezea Mtibwa Sugar kwa miaka miwili tangu alipojiunga nayo akitokea Taasisi ya Soka Tanzania (TSA) ambako alikuwa pamoja na Thomas Ulimwengu alisema kwamba amefurahi kutua Msimbazi.
“Nimefurahi sana kuja Simba SC, ni ndoto zangu za muda mrefu na sasa ni wakati wa kufanya kazi tu,”alisema.

No comments:

Post a Comment