HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 16 November 2013

SARE YAWAPELEKA IVORY COAST BRAZIL "YAUNGANA NA NIGERIA"



 

TIMU ya taifa ya Ivory Coast imefuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia baada ya sare ya 1-1 usiku huu ugenini na Senegal kwenye Uwanja wa Mohamed V in Casablanca, Morocco. 

Matokeo hayo yanaifanya Didier Drogba na wenzake wafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-2 na kuungana na Nigeria iliyoitoa kwa jumla ya mabao 4-1 Ethiopia.

Ikiwa inajivunia ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza, Tembo walilazimika kusota kusawazisha bao baada ya Moussa Sow kutangulia kuwafungia Simba wa Teranga kwa penalti, kabla ya Salomon Kalou kusawazisha dakika za majeruhi.
Kikosi cha Senegal: Coundoul, S. Sane, L. Sane, Mane, Badji/Saivet dk82, P. Cisse, Mbodji, Gueye, Souare, Djilobodji na Ndoye/Sow 66.
Ivory Coast: Barry, K. Toure, Bamba, Gosso, Zokora, Romaric, Aurier, Y. Toure, Kalou, Gervinho/Sio dk80 na Drogba

No comments:

Post a Comment