BLATTER DHIDI YA UBAGUZI
RAIS wa
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter anataka adhabu kali zaidi ili
kupambana na ubaguzi katika soka ikiwemo adhabu ya kuondoa timu mashindanoni au
kuwakata alama (POINT).
Kauli ya
Blatter imekuja kufuatia Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuanza uchunguzi
dhidi ya klabu ya CSKA Moscow baada kiungo wa Manchester City Yaya Toure
kulalamika kufanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki.
Blatter amesema
faini inayotozwa na timu kucheza bila mashabiki inaonekana ni adhabu
isiyotosheleza kwasasa. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kama kweli
wanataka kutokomeza suala hilo michezoni basi inapaswa adhabu kali zaidi kama
kuondoa timu katika mashindano husika au kuzikata alama ziongezwe kwenye sheria
ili kudhibiti mashabiki wasio na adabu.

No comments:
Post a Comment