HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 27 October 2013

WANAWAKE MARUFUKU KUENDESHA MAGARI SAUDIA




Polisi Saudi Arabia imesema kiasi ya wanawake 16 wametozwa faini kwa kuendesha magari katika siku ambayo ilitengwa  rasmi na wanaharakati kuipinga sheria inayowakataza wanawake kuendesha magari katika taifa hilo la kifalme.

Wanawake kadhaa walijitokeza katika miji mbali mbali nchini humo siku ya jumamosi kuunga mkono mwito wa wanaharakati uliotolewa kupitia mitandao. Naibu wa polisi katika mji mkuu wa nchi hiyo,Riyadh, Fawaz al-Miman, amesema polisi  iliwasimamisha wanawake sita waliokuwa wanaendesha magari  mjini humo na kuwatoza faini ya riyali 300 sawa na dola 80 kila mmoja.

Mjini Jedddah msemaji wa polisi katika eneo hilo Nawaf al-Bouq amesema wanawake wawili pia walitozwa faini kwa makosa ya kuendesha gari. Wakati huo huo magazeti ya Saudi Arabia yameripoti pia wanawake wengine sita walisimamishwa na polisi katika mkoa wa Mashariki huku wengine wakisimamishwa katika maeneo mengine nchini humo.

No comments:

Post a Comment