Dr Slaa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) hakijawasilisha taarifa zake za mapato na matumizi inayoonesha
ilivyotumia fedha za ruzuku inayopewa na serikali kwa ajili ya kufanyiwa
ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kama
kilivyokuwa kimedai
.
Katika taarifa yake Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliyotoa jana kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC), vyama vilivyowasilisha taarifa za hesabu zake kwa
Msajili ni vinne.
Vyama hivyo ni Chama cha Wananchi
(CUF), Chama Cha Mapinduzi(CCM), Chama cha Tanzania Labour (TLP) na
NCCR-Mageuzi.
Awali katika taarifa yake Chadema
ilidai kuwasilisha taarifa zake za fedha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na
zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12.
Chama hicho kilisema kina uthibitisho
na barua ya Msajili wa vyama yenye kumb. Na CDA.112/123/01a/37 ya Septemba 4,
2012, iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa.
Uthibitisho huo ulitolewa kukanusha
taarifa ya Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, iliyosema kuwa vyama vya siasa vinavyopata
ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa
ajili ya kufanyiwa ukaguzi na CAG, kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

No comments:
Post a Comment