La liga
Messi na Neymar
|
EL CLASICO: BARCA 2 REAL 1
NOU CAMP ilikuwa ni
furaha tupu baada ya FC Barcelona kuwachapa Wapinzani wao wakubwa huko Spain,
Real Madrid, Bao 2-1 katika Mechi ya La Liga ambayo imewafanya wabakie
kileleni.
Kipigo hiki
kimewabakiza Real Madrid Nafasi ya 3 sasa wakiwa Pointi 6 nyuma ya Barcelona.
Barca ndio walianza
kufunga kwa Bao la Kijana wao mpya kutoka Brazil, Neymar, ambae baada ya kupata
pasi kutoka kwa Andres Iniesta alipiga hatua kadhaa na kuachia kiki ya chini
iliyomparaza Beki wa Real Pepe na kumhadaa Kipa Diego Lopez.
Katika Dakika ya 78,
Alexis Sanchez aliifungia Barca Bao zuri baada kupiga Mpira wa juu uliomzidi
kimo Kipa Lopez na kutikisa nyavu.
Real walipata Bao lao
moja katika Dakika za nyongeza mfungaji akiwa Jese Rodriguez alietokea Benchi
alipopiga kiki ya chinichini baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Cristiano
Ronaldo.
Hakika Mechi hii
ilikuwa ni burudani nzuri kwa Wapenda Soka.
VIKOSI:
Real
Madrid: Lopez, Carvajal,
Ramos, Varane, Marcelo; Pepe, Khedira; Bale, Modric, Di Maria, Ronaldo.
Akiba: Casillas,
Coentrao, Benzema, Arbeloa, Jese, Isco, Illarramendi.
Barcelona:
Valdes, Alves, Pique, Mascherano,
Adriano; Busquets, Xavi, Iniesta; Messi, Fabregas, Neymar.
Akiba: Pinto,
Montoya, Song, Puyol, Sergi Roberto, Pedro, Alexis.
MSIMAMO-Timu
za Juu:
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|

No comments:
Post a Comment