HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 17 May 2018

TANGA: SH MIL 279 ZATUMIKA KUJENGA VYUMA 11 VYA MADARASA SHULE YA MSINGI BOMBO

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia akimuonyesha kitu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya
kuzindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 55 kwenye Jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi  ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.

Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.


Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule
ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma.

Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi
cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili
kupitia sekta hiyo.

“Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo
yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila
kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali
inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana nanyi”Alisema.
 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo

“Lakini pia kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha
hizo zinasaidia kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi
wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa watoto wetu elimu bora “Alisema.

Awali akizungumza katika ufunguzi huo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga
alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyotumia zaidi ya milooni 279
zilitokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kuongezewa na serikali.
Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo wana mpongeza Rais Dkt John
Magufuli kupitia Wizara ya Elimu kuweka msukumo wao ambapo alihaidia
kuzungumza na Waziri wa Wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio wakapata na kupokea kiasi cha milioni 136.6.

“Katika suala hili naomba nikupongeze sana Mh Waziri Ummy kwa
kulipigania Jiji la Tanga ndani na nje kuhakikisha wananchi wanaondokana
na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hivyo nisema
tutaendelea kushirikiana”Alisema.


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi
aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa
kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili
wananfunzi waweze kuendelea na masomo.

“Tunaishukuru Serikali kwa kusaidia ujenzi huu lakini Mh Waziri Ummy kwa
msukumo mkubwa uliouweka kwenye jambo hilo kwani shule waliokuwa
wamehamia ya Mkwakwani walikuwa na msongamano mkubwa na kusababisha kutokupata matokeo mazuri “Alisema

"KAMA UNADAIWA NA JESHI NA ULIPI HIYO NI DHARAU" NATOA MIEZI MITATU; RAIS MAGUFULI


Rais John Magufuli ametoa  mwezi mmoja kwa taasisi za  Serikali na watu binafsi wanaodaiwa Sh 41.4 billioni na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuhakikisha wanalipa fedha hizo.

Magufuli ametoa maagizo hayo leo Alhamisi Mei 17, 2018 alipokuwa akizindua kituo cha uwekezaji  cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), jijini Dar es Salaam.

Ametoa maagizo hayo baada ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo kumuomba kiongozi mkuu huyo wa nchi kusaidia kulipwa kwa madeni hayo.

Awali,  Mabeyo alimueleza Rais kuwa changamoto waliyonayo ni kutolipwa madeni na watu wanaofanya nao kazi.

Amesema kupitia Suma JKT walitengeneza na kukopesha watu mbalimbali na matrekta yenye thamani ya Sh40bilioni na zilizolipwa ni Sh2 bilioni na kubaki deni la Sh 38bilioni.

Ameeleza pia Suma JKT wanaolinda taasisi za Serikali wanadai  Sh 3.4 billion,  hivyo kufanya madeni hayo kwa Sh 41.4 billioni.

 "Tunaomba utusaidie kutia msukumo katika hili kwa sababu taasisi za Serikali zina lugha ya tutalipa tu endeleeni na ulinzi tu" amesema Mabeyo.

Mabeyo amesema kuwa kutokana na hali hiyo wanashindwa kuwalipa pamoja na gharama nyingine za kujikimu.

 "Waziri wa Ulinzi,  Katibu mkuu wa wizara ya Ulinzi waandikieni barua na mnitumie nakala ili niwe nafuatilia watakapokuwa wameanza kulipa.  Nataka fedha hizo zipatikane ili ziweze kutumika kujenga viwanda vingine ."amesema Magufuli akijibu maombi ya Mabeyo.

"Mtu anaanzaje kuacha kulipa fedha ya jeshi,  hii  ni  dharau kubwa,  raia wadharauliwe na Jeshi pia?”

“Niwaombe wote wanaodaiwa madeni kwa kuchukua matrekta, mimi niwape mwezi mmoja. ndani ya mwezi mmoja wawe wamelipa, baada ya mwezi mmoja vyombo vyote vya ulinzi na usalama vianze kuwasaka wote.” 

Katika hatua nyingine; Magufuli ameagiza kuwa apelekewe majina ya maofisa waandamizi wa jeshi wastaafu ili awateue kwenye bodi mbali mbali.

"Nileteeni majina yao kwani napata shida kuteua viongozi wa bodi kutokana na tatizo la uadilifu wao. Lakini hawa bado wana uadilifu na nidhamu ya kutosha na bado vijana ambao sidhani kama yupo atakayekataa nikimteua atusaidie,” amesema.

MBUNGE WA CHADEMA AUGUA GHAFLA, KESI YAKE YAAHIRISHWA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro imeahirisha kesi ya tuhuma za kuchoma ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Sofi baada ya mshtakiwa wa kwanza, Suzan Kiwanga kuugua ghafla.

Kabla ya kuhairishwa kwa kesi hiyo leo Alhamisi Mei 17, 2018, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali,  Sunday Hyera ulionekana kutokubaliana na taarifa hizo za ugonjwa.

Hali hiyo ilimfanya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ivan Msack kumtaka mdhamini pamoja na wakili wa upande wa utetezi, Barthelomew Tarimo kuwasilisha taarifa ya daktari itakayothibitisha taarifa hizo za ugonjwa.

Wakili Tarimo na mdhamini wa Kiwanga walitoka na kwenda kuchukua taarifa hiyo ya daktari wa kituo cha afya cha Aga khan iliyoeleza kuwa Kiwanga anasumbuliwa na kichwa na maumivu ya mwili na kuiwasilisha mahakamani.

Katika taarifa hiyo ya daktari ilieleza kuwa Kiwanga amepumzishwa kwa saa sita na hivyo Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Mei 18 mwaka huu.