Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
kulia akimuonyesha kitu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya kuzindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi. |
Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.
Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule
ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma.
Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi
cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili
kupitia sekta hiyo.
“Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo
yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila
kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali
inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana nanyi”Alisema.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo |
“Lakini pia kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha
hizo zinasaidia kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi
wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa watoto wetu elimu bora “Alisema.
Awali akizungumza katika ufunguzi huo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga
alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyotumia zaidi ya milooni 279
zilitokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kuongezewa na serikali.
Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo wana mpongeza Rais Dkt John
Magufuli kupitia Wizara ya Elimu kuweka msukumo wao ambapo alihaidia
kuzungumza na Waziri wa Wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio wakapata na kupokea kiasi cha milioni 136.6.
“Katika suala hili naomba nikupongeze sana Mh Waziri Ummy kwa
kulipigania Jiji la Tanga ndani na nje kuhakikisha wananchi wanaondokana
na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hivyo nisema
tutaendelea kushirikiana”Alisema.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi
aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa
kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili
wananfunzi waweze kuendelea na masomo.
“Tunaishukuru Serikali kwa kusaidia ujenzi huu lakini Mh Waziri Ummy kwa
msukumo mkubwa uliouweka kwenye jambo hilo kwani shule waliokuwa
wamehamia ya Mkwakwani walikuwa na msongamano mkubwa na kusababisha kutokupata matokeo mazuri “Alisema
No comments:
Post a Comment