HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 22 December 2017

WANAOISHI NA VVU TANGA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA IMANI ZA KISHIRIKIKA


Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) mkoani Tanga wametakiwa kuachana na kasumba za kukimbia kwa waganga wa kienyeji na  kuendelea na utaratibu walipangiwa na wahudumu wa afya wa kutumia dawa  kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia matatizo makubwa.

Hayo yalisemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt Asha Mahita (Pichani) wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo Waviu washauri ili waweze kuunganisha jamii kwenda katika vituo vya afya. Warsha hiyo inaratibiwa na Shirika la AGPAHI mkoani hapa.

Alisema vitendo vya wagonjwa kuacha dawa vinaweza kuwaweka kwenye wakati mgumu ikiwemo kupata usugu ambao unaweza kupelekea kupoteza maisha kutokana na kushindwa kufuata utaratibu uliowekwa na kuwataka kuondokana na tabia za namna hiyo.

“Kuna tabia ambayo imejengeka baadhi ya wagonjwa kuacha kutumia dawa na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kwani wanapoacha kutumia dozi na kutumia dawa nyingine.. virusi vinakuwa na usugu hali inayowasababishia hali mbaya zaidi na hata uwezekano wa kupoteza maisha “Alisema.

“Mpaka watu watambue kuwa hakuna dawa iliyothibitishwa kutibu VVU hivyo waendelea kuzitumia dawa za kupunguza makali ya VUU (ARV) ikiwemo kuacha kwenda kwa waganga wa kinyeji kwani wanaweza kukumbana na matatizo makubwa sana “Alisema.

Aidha alisema pia katika mpango wa mkoa wa Tanga wataendelea kuhamasisha wananchi kwenda kwenye vituo vya afya ili waweze kujua afya zao ikiwemo kuweza kuchukua hatua iwapo watabainika wameathirika.

“Lakini pia kwa watoto maana upimaji wao upo chini ikiwemo kuhakikisha watoto wanaopata maambuzi wanaanzishiwa dawa mapema kwani zitawasaidia kuongeza maisha yao na kuishi na afya njema”Alisema. 

Awali akizungumza katika semina hiyo,Afisa Mradi Huduma Unganishi wa Jamii wa Shirika la AGPAHI mkoani Geita Richard Kambarangwe alisema warsha hiyo ni kuwapa elimu zaidi Waviu washauri wanaosaidia kutoa huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC) kwa watu wanaoishi na VVU.

Alisema pia kuweza kuwasaidia kupata ujuzi zaidi ili kujifunza mbinu za kuwatafuta na kuwaunganisha wateja wa CTC na vituo kwa jamii kuweza kupunguza idadi ya kupotea kwa wateja.

“Lakini pia takwimu za Tanzania na mkoa inaonyesha watu wengi wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU wanaweza kupotea kwenye huduma hivyo shirika la AGPAHI mara kwa mara linazingatia kutoa elimu  itakayowasaidia watu kupata uelewa wa lishe na matumizi sahihi ya dawa “Alisema.

No comments:

Post a Comment