HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 22 December 2017

MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2017 SASA YAFUTWA RASMI.


WAANDAAJI wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Kampuni ya Lino International Agency Limited,  wamesema  kwamba hakutakuwa na Fainali za Taifa za shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2017.


Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo imeeleza kuwa sababu kubwa ya kuahirishwa kwa shindano hilo ni ukosefu wa Wadhamini ambao kwa njia moja au nyingine huwezesha kufanyika kwa mashindano hayo kwa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo zawadi za washiriki.

Aidha waandaaji hao pia wamesema kuwa kuchelewa kupata kibali cha kuanza mchakato wa Miss Tanzania 2017, ambacho kilitolewa na BASATA mwezi Septemba mwaka huu pia kimechangia kukosa kwasababu muda ulikuwa umeshaenda.

Mashindano ya kutafuta warembo wa Miss Tanzania yamekuwa yakifanyika kila mwaka na baadae kuibua mastaa mbalimbali kama Wema Sepetu, Lulu Diva, Jokate Mwegelo na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment