HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 17 February 2017

ZAIDI YA MILIONI 300 KUTUMIKA KUJENGA MACHINJIO YA KISASA PONGWE TANGA.



HALMASHAURI ya Jiji la Tanga inatarajia kutumia zaidi ya shilingi
Milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mradi mpya wa machinjio ya kisasa yatakayojengwa katika maeneo ya Pongwe Jijini hapa yatakayoendana na ukuaji wa Jiji na ongezeko la watu tofauti na machinjio yaliyopo sasa ambayo hayakidhi viwango bora.


Hayo yamezungumzwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustafa
Seleboss kuwa lazima viongozi wabadilike kiutendaji na kuwepo na
maboresho makubwa katika huduma mbalimbali ambazo zinatija kubwa kwa maendeleo ya Jiji na afya za wananchi.

Aidha alisema kumekuwepo na malalamiko kwa muda mrefu hasa kwa wafanya biashara wa nyama yanayodai maboresho katika machinjio yaliopo sasa ya sahare kutokana na miundombinu yake kuwa ni ya kizamani na mazingira mabovu kwa shughuli hizo za uchinjaji wa wanyama kama ng’ombe,mbuzi na kondoo.

“Hakuna sababu ya kukwepa ukweli unaozungumzwa na wananchi,Tanga
kunahitajika nguvu ya ziada ili kukabiliana na maboresho ya miradi
mingi kama si kujenga upya,ukiangalia machio yaliyopo hayaendani na
hadhi ya Jiji lazima tuwekeze kwa nguvu zote ili tutoke hapa tulipo na
kupiga hatua zaidi kama ilivyo kwa Majiji mengine”Alisema.

Katibu wa chama cha Wachinjaji wa Ngombe Jijini Tanga, Hassani Mohamed alizungumza na Tanzania Daima ilipotembelea katika machinjio hayo na kubainisha kuwa hali ya machinjio hayo sio nzuri kyokana na
miundombinu yake kuwa ya kizamani na kusasabisha kero kubwa kwa
watumishi na wafanyabiashara wa ng’ombe.

Alisema licha ya kuwepo kwa suala hilo lakini hata eneo ambalo
limekuwa likishushiwa ng’ombe na kuhifadhia  yamekuwa mabovu kwa muda mrefu bila kutengenezwa jambo ambalo linapelekea eneo hili kuwa na kikwazo wakati wa ushushaji wa mifugo hiyo.

Hali hiyo inasababisha wakati mwengine ng’ombe wanaopelekwa kwenye
machinjio hayo kukimbia wakati wakishushwa na hivyo kusababisha hatari
kwa wakazi wa maeneo jirani,wachungaji na hata wafanyajkazi  hivyo
kuomba kujengwe fensi kwenye eneo hilo ili kudhibiti.

Mmoja ya wafanyabiashara wa ng’ombe Jijini Tanga Ally Rashid alisema
mazingira ya machinjio hayo si mazuri kutokana na kuwepo na majengo ya
kizamani,machinjio hayo kuzungukwa na majani mengi na ni hatari kwa
kiafya za wanachi ambao ndio walaji wa nyama inayotoka katika
machinjio hayo.

Aidha alisema Halmashauri inapaswa kuangalia namna ya kuimarisha
barabara ya kuelekea kwenye machinjio hayo kutoka kwenye barabara kuu
inayoelekea eneo la Sahare ili kurahisisha upitikaji wake kwa nyakati
zote bila kuwepo na usumbufu.

Alisema ongezeko la uchinjwaji wa ng’ombe,mbuzi na kondoo linaongezeka
kila siku kutokana na ukuaji wa Jiji jambo ambalo linasababisha
msongamano wa wanyama hao kutokana na kutokuwepo kwa eneo la
kutosha,wigo na sehemu ya kuhifadhia ng’ombe kabla ya kuchinjwa.

No comments:

Post a Comment