Jaji mmoja wa Marekani
amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia
kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini
Marekani.
Jaji
wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na
kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea
kusikilizwa mahakamani.
Serikali
inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni
changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.
Serikali
ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais
Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini
Marekani juma lililopita.
Kutokana
na hatua hiyo, Idara ya Forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege
kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa
ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye
Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.
Wakati
huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema kuwa
alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika tukio alilosema
ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran katika paspoti yake.

No comments:
Post a Comment