
Mwenyekiti wa Chama cha
wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekanusha tuhuma za kuwa na ukaribu
unaotia shaka kati yake na serikali na kutolea ufafanuzi ishu mbalimbali
zinazoashiria ukaribu huo ikiwemo ya kuchepusha ruzuku ya chama.
Mwenyekiti
huyo anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kinachodaiwa kuwa ni
ukaribu wake na serikali, siyo sahihi kwa kuwa yeye huwa anaalikwa tu kwenye
matukio mbalimbali ya kitaifa ambayo hawezi kukataa mwaliko.
"Kwa
mfano ukikaribishwa kwenye shughuli ya serikai, labda Rais anazindua kitu, au
sherehe za kitaifa na Rais yupo utakataaje" Amesema Lipumba.
RUZUKU
Suala
la ruzuku ya chama hicho kuchepushwa pia ni jambo linalodaiwa kuwa ushahdi wa
Prof Lipumba kuwa karibu zaidi na serikali, ambapo amesema ilikuwa ni lazima
iwe hivyo kutokana na uamuzi wake kama Mwenyekiti wa chama wa kutengua uteuzi
wa Mkurugenzi wa Fedha, ambaye ndiye aliyekuwa mtia sahihi katika masuala ya
fedha.
Pia
sababu nyingine ya kuchepusha fedha za ruzuku amesema ni mahitaji ya chama kwa
kuwa kilikuwa kinaingia kwenye uchaguzi hivyo kilihitaji fedha kwa ajili ya
shighuli mbalimbali.
"
Kuhusu ruzuku, nilikuwa nimetengua uteuzi wa mkurugenzi wa fedha, bwana
Bashange, kwahiyo hakuwa tena signatory wetu, kwa nafasi yangu kama mwenyekiti
niliona hafai, tukajitahidi kufungua akaunti nyingine lakini haikuwezekana.
Ikabidi Naibu Katibu Mkuu ambaye ndiye anayeshika nafasi ya Katibu Mkuu
anapokuwa hayupo ofisini, aandike barua ya kuomba ruzuku kwa ajili ya mahitaji
tuliyokuwa nayo"Ameeleza
Lipumba
Lipumba
ameendelea kusema "Tukapeleka taarifa kuomba ruzuku. Kwahiyo Naibu
Katibu Mkuu akaandika barua kwenda kwa Msajili kuwa tunaomba ruzuku na ipitie
kwenye akaunti nyingine, na hilo likafanyika"
MIKUTANO
Kuhusu
yeye kuruhusiwa kufanya ikutano, huku Katibu Mkuu wake akizuiliwa, hususani
tukio lililotokea mkoani Mtwara, Lipumba amesema hata yeye alipokwenda Mtwara
hakuruhusiwa kufanya kilichokuwa kimempeleka, na badala yake aliishia kufanya
mikutano ya ndani, huku akibainisha kuwa kilichomkwamisha Maalim Seif ni kwenda
bila kutoa taarifa kwa kiongozi wa wilaya.
"Nimekwenda
Mtwara, nilikaribishwa na viiongozi wa wilaya, kazi yangu ilikuwa ni kufungua
matawi, lakini polisi wakanizuia kuwa sitakiwi kufanya mikutano ya nje, nikafanya
mikutano ya ndani...Lakini Maalim Seif alikwenda bila kumtaarifu kiongozi wa
wilaya". Amesema
ULINZI
Lipumba
aliyekuwa katika mahojiano na kituo kimoja cha TV, amekanusha taarifa za kupewa
ulinzi na serikali na kufafanua tukio la kupigiwa saluti na askari, akisema
kuwa siku hiyo hakupigiwa yeye saluti bali diwani wa eneo ambalo yeye
alishiriki kufanya usafi.
"Pale
Buguruni, tulikuwa katika usafi, na tulikuwa na diwani wa eneo lile, askari
walikuwa wakiangalia usalama, na alipotokea diwani wa eneo lile, askari
walimpigia yeye kwa kuwa ndiye mkuu wa eneo lile, siyo mimi"
Kitendo
kilichodaiwa kuwa ni askari kumpigia saluti Prof Lipumba
Katika
hatua nyingine, amesema anaendelea kumtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu
halali wa CUF, huku akimtaka amfuate ili wamalize tofauti zao na kufanya
kazi kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment