
Urusi imeonya kwamba italipiza kisasi hatua ya rais wa
Marekani Barrack Obama ya kuwatimua wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma
kwamba Urusi iliingilia maswala ya uchaguzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa
mitandaoni.
Obama
amesema Urusi pia imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani.
Kwa
upande wake, rais mteule Donald Trump ambae mara kwa mara amekuwa akizipuuzilia
taarifa hizo za udukuzi, sasa amesema atakutana na wakuu wa kiintellijensia wa
Marekani ili kupata undani zaidi wa swala hilo.
Msemaji
wa rais Vladmir Putin amesema kuwa hatua zitakazochukuliwa na Urusi zitaiathiri
Marekani.
Hatahivyo
amesema kuwa Urusi itasubiri hadi rais mteule Donald Trump ambaye amepinga
tuhuma hizo za udukuzi atakapochukua mamlaka.
Urusi
imekana madai yoyote ya udukuzi na kuvitaja vikwazo hivyo vya Marekani kama
visivyo na msingi.
Siku
ya Alhamisi, Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ilitangaza kwamba
mabalozi hao 35 kutoka Urusi pamoja na wasaidizi wao huko San Fransisco
hawatakiwi Marekani na kuwapatia wao na familia zao muda wa saa 72 kuondoka
nchi humo.
No comments:
Post a Comment