HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 23 December 2016

HAYA NI MAJIBU YA WIZARA YA ELIMU KUHUSU AJIRA ZA WALIMU.



 Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imesema haihusiki na utoaji wa ajira za walimu nchini, isipokuwa inachokifanya ni uhakiki wa taarifa za walimu wenye sifa za kuajiriwa serikalini.

Akizungumza nakituo cha  EATV jana, Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya (pichani juu) amesema kuwa kwa sasa wizara hiyo inapitia taarifa (CV) za walimu waliohitimu ngazi ya Stashada na Stashahada, na baada ya hapo itazituma taarifa hizo katika Wizara ya Utumishi ambao ndiyo wanaohusika na kuajiri.

Akizungumzia sababu za kuwatenga wahitimu wa ngazi ya cheti, Manyanya amesema uhitaji mkubwa uliopo kwa sasa ni kwa walimu wa sekondari hususani wa masomo ya Phisics, Hisabati, Chemistry na Biolojia, hivyo inawahitaji kwa haraka zaidi walimu hao huku akisema wahitimu wengine ambao siyo wa masomo hayo na ambao siyo kwa ajili ya kufundisha sekondari, wasubiri utaratibu wa wizara inayohusika na utumishi.

"Siyo kwamba hatuhitaji walimu wa shule za msingi, lakini uhitaji mkubwa tulionao kwa sasa ni walimu wa sekondari, sisi hatuajiri, sisi tunafanya uhakiki, na sasa tunapitia CV za wahitimu waliotuma taarifa zao, tukishajiridhisha na wale ambao taarifa zao ni sahihi na wana sifa tunazohitaji, tunazipeleka Utumishi, hao ndiyo wataajiri, halafu majina yatapelekwa TAMISEMI kwa ajili ya kupangiwa maeneo ya kazi" Amesema Manyanya

Kuhusu idadi ya walimu wanaohitajika haraka, Manyanya amesema, wanahitajika walimu wengi kuliko idadi waliyoitoa mwanzo, na kuwataka wote waliotuma taarifa zao wawe na subira kwa kuwa mchako wa uhakiki bado unaendelea na majina yatatangazwa muda mfupi ujao ambao hautazidi kipindi cha miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment