
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikia kukusanya shilingi trilioni 1.15 kwa mwezi
Oktoba ikiwa ni kukamilisha malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi Bw. Richard Kayombo (PICHANI JUU)wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hali ya makusanyo na
zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN)linaloendelea hivi
sasa.
“Tumefanikiwa kukusanya shilingi
Trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni kufanikisha malengo ya
ukusanyaji kodi nchini ili kukuza uchumi wa nchi pamoja kusaidia Serikali
kuendeleza huduma za jamii nchini” alisema
Bw. Kayombo.
Aidha Bw. Kayombo amesema kuwa mapato
hayo yametokana na mikakati thabiti iliyowekwa na mamlaka hiyo katika
ukusanyaji kodi hapa nchini ili kuweza kusaidia ongezeko la pato la Taifa .
Katika hatua nyingine TRA
imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa zikiendelea katika mahakama
mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake na kufanikiwa kupata kiasi cha
takribani Bilioni 16.9 .
“Tumefanikiwa kushinda kesi 9 kati
ya 10 ambazo zilifikishwa mahakamani dhidi ya walipa kodi na kupata kiasi cha
shilingi bilioni 16.9 hivyo kufanya juhudi zetu za kukusanya mapato mengi
zaidi” aliongeza Bw. Kayombo.
Mbali na hayo Bw. Kayombo amesema
kuwa zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi ambalo limeanza
hivi karibuni linaendelea na litafikia tamati Novemba 30 mwaka huu kwa mkoa Dar
es salaam hivyo wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uhakiki huo.
Aidha Bw. Kayombo ameongeza
kuwa kila mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi anatakiwa akahakiki
kwa ajili ya kupata taarifa sahihi za mlipa kodi ili kuepuka kufutwa kwa
namba yake ya utambulisho baada ya zoezi hilo kumalizika kwa mkoa husika.
No comments:
Post a Comment