Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli leo tarehe 24 Agosti, 2016 amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa.Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Modestus Francis Kipilimba
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye amestaafu.Dkt.
Modestus Francis Kipilimba anaapishwa leo mchana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw.
Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.Kabla ya
uteuzi huo Bw. Robert Msalika alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania
nchini Ethiopia.
Wakati huo huo, Rais Magufuli
amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw.
George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.Wakurugenzi
na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi
zao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Dar es Salaam
24 Agosti, 2016
No comments:
Post a Comment