HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
Pages
Thursday, 21 July 2016
HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YALAUMIWA KWA UBOVU WA BARABARA ZAKE.
Baadhi ya Madereva wa daladala pamoja na Wananchi wa jiji la Tanga wameilalamikia halmashauri ya jiji hilo kwa kushindwa kukarabati miundombinu ya barabara kwa kipindi kirefu hivyo kuwachanzo cha ajali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao Jana wamesema kuwa kutokarabatiwa kwa miundombinu ya barabara kwa kipindi kirefu ndio chanzo kikubwa cha ajali za barabarani ambazo zinaendelea kugarimu maisha ya Watanzania wengi hivyo kuiyomba halmashauri ya jiji kutengeneza miundo hiyo.
Kwaupande wake Mhandisi wa jiji la Tanga Afeilile Lamsy amesema kuwa barabara nyingi zilizo kuwa na mashimo ni kutoka na mvua za masika zilizo kuwa sinanyesha maeneo mengi nchini hivyo kama halmashauri inampango wa kuzifanyia marekebisho barabara hizo.
Aidha Mhandisi wa jiji amewataka wanainchi kuwa wavumilivu na kuendelea kutunza miundo mbinu kwa kufuata kanunu na sheria wakati serikali ikiendelea kukalabati barabara ambazo zimekuwa korofi kwa watumiaji .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment