MMILIKI wa Klabu ya Chelsea Roman
Abramovich amewaambia Wachezaji wa Klabu hiyo kuwa Antonio Conte ndie atakuwa
Meneja mpya Msimu ujao kwa mujibu wa ripoti toka Italy.
Kwa
mujibu wa Jarida la Italy, Corriere dello Sport, Abramovich amewahakikishia
Wachezaji wa Chelsea kuwa Conte ndie Meneja mpya wakati alipokutana na Kikosi
chote kwenye Kituo cha Mazoezi cha Timu hiyo huko Cobham Mjini London.
Hivi
sasa Chelsea wana Meneja wa muda Guus Hiddink ambae Mkataba wake unamalizika
mwishoni mwa Msimu baada ya kuteuliwa kuchukua nafasi ya Jose Mourinho
alieondolewa Mwezi Desemba.
Tangu
wakati huo, Hiddink ameisimamisha wima Chelsea na kupanda kwenye Ligi Kuu
England hadi Nafasi ya 10 toka Nafasi za mkiani Mwezi Desemba ikiwa sasa Pointi
8 tu nyuma ya Timu ya 4 kwenye Ligi.
No comments:
Post a Comment