Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, ameweka bayana sababu
ya kuweka kambi jijini Tanga kuwa ni kutaka kujenga ‘fiziki’ na kuwaongezea
kasi wachezaji wake.
Katika maandalizi hayo, Hall amesema
amepanga kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Mgambo na African Sports
lakini akaweka sababu za kuzichagua mechi hizo badala ya Coastal kwa kusema
anataka kuzisoma mapema kabla ya kukutana nazo kwenye mechi zijazo.
“Ukiangalia hatujakutana na timu
hizi, tuna mchezo na Mgambo hapahapa Mkwakwani kama ilivyo kwa African Sports
pia hatujacheza nao, kwa hiyo niliona kuna kila sababu ya kuziona kipindi hiki
kabla ya kukutana kwenye mechi zenyewe.
Azam FC jana ilicheza mechi ya
kirafiki na kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Mgambo Shooting ikiwa ni mechi
yake ya kwanza baada ya kuweka kambi hiyo ya Tanga.
Wiki ijayo, Azam itakipiga na Simba
katika Ligi Kuu Bara, kisha kuwafuata Majimaji mkoani Ruvuma, kabla ya kukipiga
na Mgambo, Januari 20, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


No comments:
Post a Comment