Mzozo wa kidiplomasia umezuka kati ya makao makuu ya papa
mtakatifu ya the Vatican na Ufaransa kuhusiana na uteuzi wa balozi mpya wa
Ufaransa, mjini Rome.
Rais wa Ufaransa
Francois Holland, amempendekeza muumini mmoja wa kanisa hilo ambaye ni mpenzi
wa jinsia moja kuwa balozi wake mjini Vatican.Lakini utawala wa Vatican umesema
uteuzi huo haukubaliki.
Makao makuu ya papa
mjini The Vatican hayajasema lolote kuhusiana na uteuzi huo ,lakini ni dhahiri
kuwa baadhi ya maafisa wakuu katika kanisa hilo hawajakubali msimamo wa papa
kuhusiana na waumini wa kanisa hilo ambao ni wapenzi wa jinsia moja.Papa
alinukuliwa akihoji kuwa yeye hawezi kumhukumu mtu yeyote kwa misingi yoyote.
Serikali ya Ufaransa
ilimteua laurent Stefanini kuwa balozi wake mjini vatican mnamo mwezi Januari
mwaka huu.
Balozi Stefanini mwenye umri
wa miaka 55,amekiri hadharani kuwa yeye anashabikia mapenzi ya jinsia moja na
amewahi kufanya kazi katika ubalozi huo mjini Roma na amekuwa mshauri wa
masuala ya kidini katika wizara ya mambo ya nje ya ufaransa.Kwa sasa hakuna
upande unaoonekana kuwa tayari kubadili msimamo wake.
Ufaransa ilhalalisha
ndoa za jinsia moja mwaka 2013 na uamuzi wa The vatican wa kukataa kumkubali
balozi Stefanini huenda ikawa ni thibitisho la The vatican la kutoidhinisha
msimamo huo wa Ufaransa.
CHANZO: BBC

No comments:
Post a Comment