MENEJA wa Manchester
United anaetoka Uholanzi Louis Van Gaal alifungwa Dabi yake ya kwanza ya Jiji
la Manchester Novemba Mwaka Jana kwa Bao la Sergio Aguero huko Etihad.
Hicho kilikuwa kipigo
cha 4 mfululizo kwa Man United mikononi mwa Mahasimu wao City lakini Van Gaal
ameapa safari hii hilo halitatokea Jumapili Uwanjani Old Trafford wakati City
watakapotua kucheza Mechi muhimu mno ya Ligi Kuu England.
Leo Van Gaal amezungumza huko
Carrington, Kituo cha Mazoezi cha Man United, na kusema: "Naiota hii Dabi,
kila Mchezaji anaota ushindi!"
Licha ya kuwa ni Dabi, lakini kama Juzi
alivyotamka Kepteni wa Man United, Wayne Rooney, kwamba ushindi unaleta kiburi
cha majivuno lakini pia safari hii kugombea 4 Bora nako ndio kunaleta
changamoto kubwa.
Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 3
wakiwa Pointi 1 mbele ya City na ushindi kwao utawapa pengo la Pointi 4 dhidi
ya City.
Van Gaal amesema: "Unataka
kushinda kwani ni hatua kubwa katika Msimamo. Ukishinda Nafasi ya 3 itapatikana
na Mwezi mmoja uliopita, ukiniondoa mimi, hakuna aliedhani hili
linawezekana!"
Kwa fomu ya sasa ilivyo, Man United
wanaingia kwenye Dabi hii wakiwa na matumaini makubwa ya ushindi baada ya
kushinda Mechi 5 mfululizo za Ligi wakati City wameshinda Mechi 2 tu kati ya 7
za Mashindano yote.
Hata hivyo, Van Gaal amesisitiza hilo
halina maana kwani hii ni Dabi na Gemu spesho.
Vile vile Van Gaal ameponda pale
alipokumbushwa historia ya hivi karibuni ya kufungwa mfululizo na City.
Amenena: "Hiyo si Historia
yangu!"
Aliongeza: "Nisemeje? Tumefungwa
1-0. Hiyo ndio historia yangu, Gemu ya mwisho tuliyocheza nao na tulipata Kadi
Nyekundu Dakika ya 39!"
Katika Mechi hiyo iliyochezwa Etihad,
Chris Smalling ndie aliepewa Kadi Nyekundu baada ya Kadi za Njano mbili.
LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 11
1445 Swansea v Everton
1700 Southampton v Hull
1700 Sunderland v Crystal Palace
1700 Tottenham v Aston Villa
1700 West Brom v Leicester
1700 West Ham v Stoke
1930 Burnley v Arsenal
Jumapili Aprili 12
1530 QPR v Chelsea
1800 Man United v Man City
Jumatatu Aprili 13
2200 Liverpool v Newcastle

No comments:
Post a Comment