KAMPUNI
ya Hall Fame Boxing imeandaa pambano la kimataifa kati ya bondia Mohamed
Matumla na bondia kutoka China, Wang Xin Hua linalotarajiwa kufanyika Machi 27,
mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema kampuni yake imeandaa pambano hilo litakalosimamiwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) na PST.
Msangi alisema wameamua kumpambanisha Matumla kwa sababu wanaamini ni bondia bora wa ngumi za kulipwa nchini na ameonesha viwango vizuri katika mapambano yake aliyowahi kucheza.
Aliongeza kuwa wanaamini bondia huyu anaweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kuitangaza kimataifa kwani ana kiwango kizuri na ana kocha mzuri.
Pia alisema katika pambano kuna baadhi ya mabondia watakaomsindikiza Matumla ambao ni Ashraf Suleiman ambaye atapambana na bondia kutoka Marekani, Joseph Rabotte, Japhet Kaseba atapambana na Mada Maugo na Karama Nyilawila atamkabili Thomas Mashali.
Kwa upande wake, kocha wa bondia huyo ambaye pia ni baba yake, Rashid Matumla alisema ameshirikiana na makocha wengine kumwandaa kutokana na pambano hili kuwa ni kimataifa, hivyo anaamini atapambana vyema na amejiandaa vizuri.
Naye bondia Mohamed alisema hapendi kuongea kwani anapenda vitendo zaidi, na kikubwa watu wajitokeze kwa wingi kuona jinsi atakavyompiga Mchina huyo.

No comments:
Post a Comment