Baada
ya kusimamishwa na uongozi wa Mbeya City, kipa David Burhan amekaribisha ofa za
kujiunga na timu nyingine ili achane na kikosi cha City FC.
Burhan, kipa wa zamani wa Tanzania Prisons FC na kipa bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13, alisimamishwa na Bodi ya Michezo ya Jiji la Mbeya kuidakia Mbeya City FC kwa madai ya kufungwa bao la kizembe na winga Mrisho Ngasa wa Yanga SC katika mechi yao iliyopita jijini Mbeya.

Mbeya City FC inayonolewa na Kocha Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Juma Mwambusi, ililala kwa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya wiki mbili zilizopita.
Ngasa
alifunga bao lisilotarajiwa katika dakika ya 59 alipounasa mpira uliokuwa
miguuni mwa kipa Burhani aliyetaka kumpiga chenga winga huyo wa zamani wa
Kagera Sugar FC, Azam FC na Simba SC.
Katika
mahojiano na mtandao huu leo jioni, Burhan amesema yuko tayari kujiunga na timu
yoyote itakayompa ofa nzuri.
Kanuni za Usajili ya FIFA zinampa idhini mchezaji kuzungumza na timu nyingine kuhusu kumsajili kama mkataba wa mchezaji husika umebakiza muda ambao si zaidi ya miezi sita.
No comments:
Post a Comment