Kwaya
ya vijana usharika wa Kana mtaa wa Duga
jijini Tanga wapo katika maandalizi yao ya mwisho ya kujiandaa kutoa mkanda wa video wa albamu yao
ijulikanayo kama vijana ni nuru ya ulimwengu.
Akizungumza
na mtandao huu mwalimu wa kwaya hiyo Atanasi Jonh amesema wanajisikia furaha kufika
hatua walionayo sasa na kusema kwao ni jambo la kujivunia.
Hata
hivyo wanatarajia kufanya harambee kwa ajli ya kupata pesa ya kuanzisha miradi
mbalimbali ambayo itawawezesha katika kuiendeleza huduma yao ya uimbaji.
“Tunamshukuru
Mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii tulionayo sasa kwani tulikuwa
tunaisubiria kwa shauku kubwa ili kuweza kutoa video yetu” Alisema John”
Aidha
amewashukuru washarika pamoja na watu mbalimbali ambao walijitoa kwa hali na
mali katika kufanikisha shughuli hiyo ambapo pia amewataka wasife moyo katika
kumtumikia mungu kaitika roho na kweli.
Aidha
amewaasa waimbaji wengine kuboresha huduma zao ili waweze kuisambaza injili ya
yesu kristo katika njia ya kweli na impasayo mungu.

No comments:
Post a Comment