MMILIKI wa Arsenal ambae ni wa Pili
kwa wingi wa Hisa zake, Alisher Usmanov, amedai msimamo wa Meneja wao Arsene
Wenger ndio unazuia Klabu hiyo kupanda juu na sasa inabidi Meneja huyo akiri
makosa yake.
Usmanov, Raia wa Uzbekistani
anaemiliki Asilimia 30 ya Hisa za Arsenal ambazo ni za pili kwa wingi wake,
ameongea mara baada ya Klabu yao kuchapwa 2-1 na Manchester United hapo
Jumamosi Uwanjani kwao Emirates.
Arsenal sasa wamepoteza Mechi 11
kati ya 15 walizocheza mwishoni na Man United na kushinda moja tu na Msimu huu
kwenye Ligi Kuu England wameshinda Mechi 4 tu kati ya 12 walizocheza.
Usmanov ametamka: “Uwezo wa Timu upo
lakini hamna mchanganuo wa kitaalam wa makosa yetu na kuyakubali. Hakuna
mwerevu yeyeto anaeweza kudumu ikiwa hakubali makosa yake. Pale ukikubali
makosa yako ndio unayaondoa. Nataka hili kwa Klabu yangu!”

Usmanov alimalizia: “Maoni yangu,
tena nayaweka bayana, tunahitaji kuimarisha kila pozisheni ili tuwe sawa na
Chelsea na Man City hapa England na Ulaya sawa na Real, Barcelona, Paris
Saint-Germain, Bayern Munich na Klabu nyingine!”
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatatu Novemba 24
2300 Aston Villa v Southampton
Jumamosi Novemba 29
1545 West Brom v Arsenal
1800 Burnley v Aston
Villa
1800 Liverpool v
Stoke
1800 Man Utd v
Hull
1800 QPR v
Leicester
1800 Swansea v Crystal
Palace
1800 West Ham v
Newcastle
2030 Sunderland v
Chelsea
Jumapili Novemba 30
1630 Southampton v Man
City
1900 Tottenham v
Everton
No comments:
Post a Comment