Mkuu wa Mkoa wa Tanga Galawa |
Na Godwin Henry Lyakurwa .TANGA
Kwa takriban Wiki
mbili sasa Wakaazi jiji la Tanga wanashuhudia kukatika hovyo kwa nishati
tegemeo ya Umeme tena pasipo taarifa Maalum kutolewa na Mamlaka
husika.(TANESCO)
Kwa takriban Wiki
mbili sasa Wakaazi jiji la Tanga wanashuhudia kukatika hovyo kwa nishati
tegemeo ya Umeme tena pasipo taarifa Maalum kutolewa na Mamlaka
husika.(TANESCO)
Mbaya zaidi ni kuwa Umeme umekuwa ukikatika muda
wa mchana,kipindi ambacho wajasiriamali huwa katika mihangaiko ya kuuza na
kuzalisha bidhaa zao kwa kutumia umeme kwa mfano mashine za kukoboa na kusaga
nafaka, Saluni za kike na za kiume, Wauzaji wa Vinywaji n.k
Sote tunatambua kuwa si wote wenye uwezo wa kumudu
gaharama za kununua Majenereta na hata wenye uwezo hujikuta wakiuza bidhaa zao
kwa bei ya juu ili kufidia gharama za mafuta ya Dizeli ambayo hutumiaka na
majnereta hayo.Kama kuna Mgao ni vyema Shirika likajikaza kisabuni kuwaita
wanahabari na kuwaeleza hali halisi ili Waathirika wajue namna ya kujisitiri
kuliko kuwaacha wakihaha wasijue Umeme utakatika muda gani.
Faida ya kujua Muda wa umeme kukatika ni kuwa Mtumiaji
ataongeza uzalishaji wakati umeme upo ili kufidia muda muda ambao umeme
hautakuwepo na hivyo kupunguza athari kwa namna moja au nyingine.
Lakini kukaa kimya kwa Mamlaka kunaibua maswali
mengi kwa watumiaji hasa wakati huu ambapo kuna shutma nzito juu ya wapi zilipo
pesa za shirika hilo ambazo ziliwekwa kwenye akaunti ya ESCROW.
Jana wakati wa mchana nikiwa katika mihangaiko ya
Siku ghafla Umeme ilikatika, tena nikiwa na taarifa za kwenda kuskan na
kuprinti, kwa kweli nilipatwa nawakati mgumu sana kwani ilinibidi nifunge
safari mpaka Jengo la Bandari ambapo kuna Jenereta ili kupata huduma hiyo kwani
Stationary nyingi hakukuwa na huduma hiyo kutokana na kukatika kwa umeme. Swali
ni Je, wale wenye mashine za kukoboa na kusaga nafaka nao wazipeleke Jengo la
Bandari.?
USIKU.Huu ni wakati mbaya zaidi kwa umeme kukatika kwani Usalama wa Watu na mali zao huwa mdogo kutoka na na uwezekano mkubwa wa kutokea kwa matukio ya wizi na Unyang'anyi wa kutumia nguvu na Silaha.
Kwa takriban Wiki
mbili sasa Wakaazi jiji la Tanga wanashuhudia kukatika hovyo kwa nishati
tegemeo ya Umeme tena pasipo taarifa Maalum kutolewa na Mamlaka
husika.(TANESCO)
Pamoja na yote hayo jiji la Tanga linae Mstahiki
Meya Omar Guledi ambaye ni msimamiaji wa Uchumi wa jiji ni vyema yeye na
Mkurugenzi wa jiji Bi Juliana Malange na kamati ya Uchumi ya jiji waketi kutafuta
utatuzi wa Janga hili kwani kuna uwezekano mkubwa biashara zikadorora na
Uzalishaji ukashuka hali ambayo itaathiri pato la Halmashauri kwa Ujumla.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Omar Guledi |
Sisi wabantu tuna misemo mingi yenye maana na hapa
niwakumbueshe Viongozi hawa ule msemo usemao, “kukaa kimya ni Ishara ya Dharau” .Watambue kuwa hakuna jambo gumu
katika ulimwengu wa sasa kama kumuongoza Mtu mwenye matatizo ya Kiuchumi kwani
muda wote atalia na wewe na mwishowe atakuharibia sio mzuri.
Mwisho..Kupitia Makala hii naomba Meneja wa TANESCO mkoani hapa awe muwazi kusema
kulikoni ili kunusuru pato la wana Tanga.
No comments:
Post a Comment