HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 30 October 2014

HUDUMA YA MATREKTA KWA WAKULIMA ZANZIBAR YABORESHWA.



Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo Zanzibar ndg Zaki Khamis Juma amesema kuwa hakuna mkulima atakaye kosa hudumua za kilimiwa na matrekta iwapo atatimiza masharti ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama kwa wakati .

Amesema kuwa Idara imejipanga vyema kupeleka matrekta kwa wakulima wa mpunga  ili kuona kwamba wakulima wote ambao watachangia gharama zinazohitajika wanapata huduma za kulimiwa mabonde yao .

Akizungumza na wakulima wakati wa  ziara yake  ya kukagua maandalizi ya kilimo cha matrekta katika mabonde ya wakulima Kisiwa Pemba , ametoa matumaini kwa wakulima ambao wamechangia gharama hizo kwamba watalimiwa kwa wakati muafaka .

Aidha amewasisitiza wakulima kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuorodhesha majina yao kwa makatibu wa mabonde ili watendaji kutoka Idara hiyo waweze kupanga idadi ya matrekta ambayo yanaweza kuhitajika katika kufanikisha lengo .

Mapema Mkuu wa Idara hiyo Pemba ndg  Amour Juma Mohammed amesisitiza kwamba Idara inatoa mafuta kulingana na idadi ya fedha ambazo zinawasilishwa kutoka kwa waratibu wa Pembejeo wa  Wilaya husika .

Katika ziara hiyo ambayo mkurugenzi ameambatana na wataalamu wa Idara ya Kilimo Pemba ametembelea katika mabonde ya Mtadoda wilaya ya Mkoani  ,Kilindi wilaya ya chake chake pamoja na bonde la Makuwini Wilaya ya Wete.

No comments:

Post a Comment